KWELI Katika picha hizi moja ni halisi na imetumika kutengeneza ngingine kwa akili unde

KWELI Katika picha hizi moja ni halisi na imetumika kutengeneza ngingine kwa akili unde

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
image.jpg
image1.jpg


​
 
Tunachokijua
Akili Unde (AI) ni seti ya teknolojia zinazoiwezesha kompyuta kutekeleza majukumu mbalimbali ya kina na kwa uwezo mkubwa kadri ya maelekezo ya mtumiaji, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kuona, kuelewa na kutafsiri lugha inayozungumzwa na maandishi, kuchanganua data, kutengeneza picha na video na kutoa mapendekezo ya utatuzi wa matatizo mbalimbali.

Aidha teknolojia hii imekuwa muhimu katika kurahisisha ufanisi wa shughuli za kila siku na hii ni pindi tu inapotumika kwa nia iliyo njema, lakini inapotumiwa kwa nia ovu huweza kusababisha madhara makubwa kwa watu, mathalani uwepo wa taarifa potofu unachangiwa pia na teknolojia hii ambayo watu hutumia kutengeneza na kusambaza taarifa zisizo sahihi mfano picha, sauti, na video.

Katika kujenga uwezo wa kumuwezesha kila mmoja kutambua maudhui yaliyotengenezwa kwa teknolojia hiyo ili kuepuka upotoshaji, wadau wa JamiiCheck walishiriki kuthibitisha picha mbili kwa kubainisha iliyotengenezwa na sababu halisi zinavyodhihirisha uhalisia huo.

Uhalisia wa picha

Muonekano wa picha zote mbili unaonesha kufanana au kuelekeana kwa kiwango kikubwa. Lakini unafahamu kuwa teknolojia ya akili unde inaweza kutumika kutengeneza au kubadili sehemu ya picha halisi na hata kusababisha kupotosha uhalisia.

Picha iliyopewa herufi 'B' pamoja na kuwa na muonekano unaofanana na picha 'A' bado mapungufu kadhaa yanayokinzana na uhalisia jambo linaloashihirisha kuhusika kwa Akili Unde katika picha 'B'.

Sehemu ya mapungufu hayo ni pamoja na uwepo wa nyumba zenye urefu usio wa kawaida ambapo zinaonesha sehemu ya paa pasipo ukuta kama nyingine zinavyoonekana, maumbo ya magari yasiyo ya kawaida pamoja na usahihi wa vimvuli ukilinganishana Picha 'A'

Aidha picha 'A' ni halisi na ndiyo iliyotumika kutengeneza picha 'B' kupitia akili unde. Kupitia utafutaji wa picha wa Google reverse image search picha hiyo ilichapishwa mtandaoni mnamo Januari 21, 2020 katika tovuti ya WIKIMEDIA COMMONS, ikionesha mandhari ya barabara ya Mbalizi - Mbeya.
​

Attachments

  • JC SHIRIKI 29JUL,25 SLD2.jpg
    JC SHIRIKI 29JUL,25 SLD2.jpg
    2 MB · Views: 28
  • JC SHIRIKI 29JUL,25 SLD3.jpg
    JC SHIRIKI 29JUL,25 SLD3.jpg
    1.9 MB · Views: 32
Kwenye hizo pichambili hakuna picha ambayo imetengenezwa kwa kutumia akili unde bali ni picha halisi ambazo zimepgwa kwenye mkoa wa mbeya

Kwa kutumia ufutiliaji wa google search images na kutumia program tumishi ya invid we verify unaonesha kuwa picha imepigwa kwenye eneo la Mbalizi Mbeya Tanzania kuonesha mandhari ya usafirishaji katika maeneo ya mipaka
picha hii imepakiwa kwenye mtandao wa kijamii kwa mara ya kwanza 21 January 2020, 10:01:47

Katika picha Barabara kuu za T8 na T10 pia zinaunganisha kupitia Mbeya, kuunganisha jiji na miji mingine na hata mpaka wa Malawi.
Pia kwa kutumia ufuatiliaji picha imechapishwa kwenye ukurasa wa Africa View Facts kwenye mtandao wa facebook ukiwa na caption ya Mbeya Tanzania .chapisho limewekwa March 4 2024 huku likiwa na takriban Maoni 56 na kusambazwa mara 36
 
Picha ya kwanza ilipigwa kwa kawaida, lakini baada ya ubora wa picha kushuka (low quality pixel), ilifanyiwa marekebisho kwa kutumia AI. Kwenye picha ya pili ...hope nimewasaidia ...ukizoom ndo utajua
 
Chukua maua yako Mkuu 👏

Chukua maua yako Mkuu 👏
Kwenye hizo pichambili hakuna picha ambayo imetengenezwa kwa kutumia akili unde bali ni picha halisi ambazo zimepgwa kwenye mkoa wa mbeya

Kwa kutumia ufutiliaji wa google search images na kutumia program tumishi ya invid we verify unaonesha kuwa picha imepigwa kwenye eneo la Mbalizi Mbeya Tanzania kuonesha mandhari ya usafirishaji katika maeneo ya mipaka
picha hii imepakiwa kwenye mtandao wa kijamii kwa mara ya kwanza 21 January 2020, 10:01:47

Katika picha Barabara kuu za T8 na T10 pia zinaunganisha kupitia Mbeya, kuunganisha jiji na miji mingine na hata mpaka wa Malawi.
Pia kwa kutumia ufuatiliaji picha imechapishwa kwenye ukurasa wa Africa View Facts kwenye mtandao wa facebook ukiwa na caption ya Mbeya Tanzania .chapisho limewekwa March 4 2024 huku likiwa na takriban Maoni 56 na kusambazwa mara 36
JamiiCheck Nashukuru kwa kutupa dokezo la mwisho.nimeona nilipo kosea ila naamini nitaendelea kufanya marekebisho na kuelewa zaidi kufanya fact checking .nnnaamini nitafanya improvements kwenye fact checking
 
Back
Top Bottom