Katika Picha: Maandamano ya wanahabari Leo

Status
Not open for further replies.

Maxence Melo

JF Founder
JF Staff
Joined
Feb 10, 2006
Posts
4,324
Reaction score
13,967
Heshima zenu wakuu,

Leo kuanzia saa 4 kamili asubuhi mpaka saa 6 kamili kulikuwa na maandamano yaa amani ya wanahabari ambayo yalianzia Mtaa wa Lugoda Jijini Dar es Salaam kuelekea Makao Makuu ya Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo. Sina nakala ya ujumbe uliopelekwa kwa waziri hapa lakini pindi nikipata nakala hiyo nitawaleteeni.

Picha na maelezo yake ni kama ifuatavyo:


Hapa ni mtaa wa Lugoda mbele ya ofisi za Business Times ambapo maandamano yalianzia. Mabango yanajieleza, siongezi kitu!

Basi midomo mingi ilionekana hivi.

Naendelea
 
Nashangaa wamekubaliana wasitaje jina la Mkuchika lakini mabango mengi yana jina hilo!

Kumbe jina la Mkuchika litaendelea kutamba pamoja na kifungo kutoisha
 
Nashangaa wamekubaliana wasitaje jina la Mkuchika lakini mabango mengi yana jina hilo!

Kumbe jina la Mkuchika litaendelea kutamba pamoja na kifungo kutoisha

huo ni upotoshaji, walikubaliana wapi wasitaje jina la Mkuchika? Kama huna uhakika walichokubaliana uliza, usijitungie unakuwa ni udaku huo.
 
Mtaandamana sana mwaka huu hata waandishi wa habari mnaowanyanyasa katika vyombo vyenu nao wataandamana kabla ya mwisho wa mwezi huu
 

Maandamano yalianza rasmi, na hapa ni mtaa wa Lugoda. Walichojibiwa nitawafahamisha punde

Naam, mabango yalikuwa yakisomeka hivi.

Na mabango mengine hivi...
 
Mtaandamana sana mwaka huu hata waandishi wa habari mnaowanyanyasa katika vyombo vyenu nao wataandamana kabla ya mwisho wa mwezi huu
Shy,

Walioandamana si wahariri pekee, nitaandika zaidi mbeleni, ngoja niweke picha kwanza halafu tutalonga mkuu
 

Sikuachiwa nipige picha tu, nikapewa bango na kufungwa mdomo kama ninavyoonekana pichani.

Kuna bango lilikuwa na ujumbe huo hapo juu...
 
hizo picha mbona hatuzioni naona umesema picha hizi hapa ziko wapi?
 

Safari ya kuelekea wizarani ilikuwa imefikia maeneo ya New Africa Hotel

Hapa maandamano yalikuwa yanakaribia wizarani kabisa
 
ohaaa nimeshaziona thanks a lot
safi sasa hii inapendeza sana walivyochukua hatua hii wahariri
 
Kumbe wakibonyezwa hulalamika.Duu wakipakazia ok.Its high time wakawa wanahariri habari kujiepusha na kufungwa midomo.Haya kubenea bado ya wenyeviti.ingawa kwa mahakama anajiamini labda anamjomba.
 

Hii sheria amekuwa akiiongelea sana Mwanakijiji, na leo ilishikiliwa bango kama inavyoonekana pichani juu
 
Kumbe wakibonyezwa hulalamika.Duu wakipakazia ok.Its high time wakawa wanahariri habari kujiepusha na kufungwa midomo.Haya kubenea bado ya wenyeviti.ingawa kwa mahakama anajiamini labda anamjomba.
Nachelea kusema mkuu, ngoja nimalize kuweka picha halafu niandike kilichoongeleka.
 
Ndio hivyo, msiposimama na kujitetea hakuna serikali ambayo ni rafiki wa waandishi wa habari, hasa pale uchafu unapokuwa mwingi kuliko usafi.
 


Yakafika Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo. Jengo hili lina wizara mbili kama inavyoonekana pichani na limeungana na CRDB Bank jirani na NIC au KCB. Nini wamekumbana nacho? Nitakufahamisheni punde
 
Nafurahia kusema kwamba ile "ndoa" kati ya viongozi wetu na baadhi ya waandishi wetu sasa imeanza kupungua kimapenzi na muda si mrefu mhimili huu wa nne utajitegemeza wenyewe.
 
Asante kwa mtiririko mwanana kabisa, hadithi njoo utamu kolea.
 
Naam, aliyeyapokea maandamano haya ni Habib Nyundo (anayeonekana pichani hapo chini) Kaimu Mkurugenzi wa Habari wa Wizara.

 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…