Bwana Kibanda (anaonekana pichani) alionekana kushangazwa na serikali kulitambua Jukwaa la wahariri la miaka ya 70 ambalo ni wazi hakuna mhariri hata mmoja aliye katika vyombo vya sasa.
[Alimwakilisha Sakina Datoo ambaye yuko masomoni Ulaya]
Alisema kuwa kinachosisitizwa na Jukwaa la Wahariri si kwamba kilichoandikwa na MwanaHalisi ni sahihi ama si sahihi lakini akatoa dodoso kuwa kuna gazeti flani la leo limeandika habari ileile japo kwa namna tofauti.
Akaendelea kushangazwa na jinsi serikali inavyoamua kuchukua hatua kali dhidi ya vyombo vya habari ilhali walimu walipogoma (kitu ambacho serikali haikukiona halali) ilikwenda mahakamani, akauliza ni kwanini serikali haikwenda mahakamani kuiomba mahakama isitishe uchapishwaji wa gazeti hilo.
Aliendelea kuonesha kusikitishwa kwake na jinsi serikali inavyoonekana kuwa na ajenda ya siri kwani aliyeongelewa ni Ridhiwani naye hakutia neno na akashangaa serikali ilifungua kinywa kwa niaba ya Ridhiwani, ikachukua hatua kwa niaba ya Ridhiwani! Alisisitiza kuwa kilichoandikwa kuhusiana na njama za baadhi ya wanachama wa CCM kuwa na mbinu za chinichini kilikuwa ni kitendo cha kisiasa na katika siasa jambo hilo lipo!
Akatanabaisha kuwa Mhariri na Mkurugenzi wa MwanaHalisi bado wanaripoti makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani kila wiki kitendo ambacho amekilaani kuwa kina kitu nyuma yake.
Aliendelea kusema kuwa baadhi ya viongozi serikalini ni wamiliki wa vyombo vya habari ambavyo vimekuwa vikipindisha habari nyingi na haviguswi. Akavitahadharisha vyombo hivyo kuwa makini kwani vinaiangusha sana sekta ya habari
Naye Ayoub Ryoba alisisitiza kuwa Uhuru wa Habari Tanzania unaendelea kukandamizwa na akasisitiza kuwa wao kama MISA hawatavumilia kuona maslahi binafsi yanalindwa na maslahi ya taifa yanawekwa kando.
Ryoba leo 28 Oct '08
Mkurugenzi wa Chama cha waandishi wanawake Tanzania (TAMWA) alionesha kutofurahishwa na kitendo cha serikali kulifungia gazeti la MwanaHalisi. Akasema ukikifungia chombo chochote cha habari ni kuwa unakuwa unawafunga wananchi midomo. Akasisitiza kuwa mwanzo wa kufungia gazeti moja ndio mwanzo wa kufungia vyombo vingine vya habari binafsi. Akasisitiza Serikali ilifungulie gazeti hilo mara moja.
Mkurugenzi TAMWA
Mimi ni mjumbe tu