Katika Serikali 3, MUUNGANO utaimarika, CCM itakufa: Hii ndo hofu na sababu CCM kukataa Serikali3

Katika Serikali 3, MUUNGANO utaimarika, CCM itakufa: Hii ndo hofu na sababu CCM kukataa Serikali3

NYAMKANG'ILI

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2012
Posts
223
Reaction score
112
CCM inataka serikali mbili ziendelee, wanakataa pendekezo la serikali 3. CCM wanatoa sababu nyingi ambazo siyo sababu hasa za kuwafanya CCM kukataa serikali3. SABABU zenyewe ZA CCM kukataa serikali3 ni hizi:

1) Muundo wa CCM, na kufanya kazi kwake, umetengenezwa kwa kuzingatia muundo wa serikali2

2) Iwapo kutakuwa na Serikali ya Tanganyika, itapaswa Rais wa Tanganyika ndiye awe mwenyekiti wa CCM taifa. Hii ni kwa sababu Tanganyika ndiko kuliko na watu wengi, raslimali nyingi, fedha nyingi, vyeo vingi vya kuwapatia makada wa chama. HILI KWA CCM ndo mtihani mkubwa, NANI AWE M/KITI kati ya Kiongozi wa TANGANYIKA na RAIS WA TZ?

3) Utulivu ndani ya CCM unategemea kitu kimoja tu: RASLIMALI na vyeo vya serikalini, katika serikali ya Jamhuri ya Muungano, ambavyo KWA MUUNDO wa sasa wa Muungano ni vya TZ, LAKINI ni vya Tanganyika katika mfumo wa serikali3. Kwa mfano, kada anapopiga kelele, anapozwa na ama uwaziri au ukuu WA MKOA, au ubalozi au u-DC, au ubunge wa kuteuliwa kama aliokuwa nao KINGUNGE kwa miaka yote, hajawahi kugombea jimboni, yeye ni mteuliwa. Na ukitofautiana nao, wanakufutia uteuzi; unarudi kijiweni, alafu baadaye unarudishwa kundini ukiwa umenyooka. Hili ndo lililotokea kwa SITTA. Hii kazi ya kujenga chama kwa kupitia mgongo wa raslimali za Tanganyika na vyeo vya Serikali anaifanya RAIS wa TZ ambaye NI M/KITI WA CCM TAIFA. Ukiiunda TANGANYIKA, BASI CCM itakuwa na mtihani mkubwa: nani awe m/kiti kati ya kiongozi wa Tanganyika mwenye mali na watu au RAIS WA TZ mwenye majeshi tu lakin asiye na mali wala watu wala vyeo vya kupooza makada?

4) Kambi za kugombea Urais wa TZ kupitia CCM. Hawa wakubwa watarudishaje pesa za 'marafiki' zao wanaowafadhili 'GIZANI' kwa ahadi za kupewa tenda, mikataba au vyeo? Hii ni kwa sababu Rais wa TZ ATAKUWA HANA vyeo wala raslimali za kuwapa makada ili watulie... HAWA WAMEJIPANGA KUKWAMISHA MCHAKATO MZIMA WA KATIBA.

Ukitazama hizi sababu (ambazo hazisemwi wala hazitasemwa hata siku moja na CCM) ndizo sababu za wao CCM kugomea serikali3. SERIKALI3 zitaimarisha sana Muungano, ila CCM itaparaganyika... na hapo ndipo wakubwa hawa wanaposema SERIKALI3 zitavunja muungano, badala ya kusema serikali3 zitaisambaratisha CCM...
 
Ila tumeshikwa pabaya na judge wetu tulidhani yu upande wetu.:crying:
 
Machadema yanataka kuvunja muungano ili yatawale tanganyika baada ya kuona ndani a muungano ni ndoto kwao kuiona ikulu
 
Tatizo la ccm inapendwa na watanzania wote.
 
Chadema iruhusu demokrasia ndani ya chama kwanza
 
Ifweero natamani nikufahamu hata kwa kukuona kwa sura wewe ni mtu wa namna gani, ila navyo hisi utakuwa unafanana na mzee majuto.
 
Muungano wa sasa unaikandamiza tanganyika zaidi, muungano wa haki ni serikali tatu au moja tu! Ccm ni maadui wa tanganyika na muungano wa dhati kabisa!
 
Mungu ibariki Tanganyika yetu irudi ili hawa wakoloni ccm walioipoteza na sasa wanaigandamiza chini Tanganyika yetu ili isichomoze waweze kuaibika na kutoweka.

Mungu ibaririki Tanganyika.
 
Ifweero natamani nikufahamu hata kwa kukuona kwa sura wewe ni mtu wa namna gani, ila navyo hisi utakuwa unafanana na mzee majuto.

Jamaa ni graduate na master pia anayo, tatizo lake njaa! Kuna kipindi rafiki yake alikuwa anamuazima gari na hela ya lunch akatanue mjini huku ili apate nafasi ya kutembea na shemeji yake(mke wa ifirwaa,)
 
niliwahi kugusia siku za nyuma kwa nini ccm hawataki serikali tatu. Hoja yangu ilifanana sana na hiyo title ya mleta thread.
 
Machadema yanataka kuvunja muungano ili yatawale tanganyika baada ya kuona ndani a muungano ni ndoto kwao kuiona ikulu

Mwaka huu mtajitia kitanzi kwani Mzee Warioba amewashika pabaya.
 
Back
Top Bottom