Katika sherehe za miaka 48 ya CCM Ludewa, mbunge ahaidi kukamilika kwa ujenzi wa shule ya sekondari mwezi Machi wanafunzi wasisafiri umbali mrefu

Katika sherehe za miaka 48 ya CCM Ludewa, mbunge ahaidi kukamilika kwa ujenzi wa shule ya sekondari mwezi Machi wanafunzi wasisafiri umbali mrefu

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Serikali imeanza kujenga shule ya Sekondari Ruhuhu wilayani Ludewa mkoani Njombe ili kupunguza adha ya watoto kusafiri umbali wa takribani Km 15 Hadi Manda Sekondari na Km 30 Hadi Mchuchuma kupata elimu.

Kwa hatua za awali Tayari madarasa mawili yapo mwishoni kukamilika na Mbunge wa Jimbo la Ludewa Joseph Kamonga anasema mwezi Machi Mwaka huu Wanatarajia wanafunzi waanze kusoma.

Katika Sherehe za miaka 48 za kuzaliwa kwa Chama Cha mapinduzi CCM mkoa wa Njombe Mkuu wa shule ya Sekondari Ruhuhu Mwalimu Enocy Dominick amesema mazingira hatarishi ya watoto wa kike kutembea umbali mrefu kwenda Manda Sekondari na wamefikia zaidi ya Asilimia 80 katika utekelezaji wake.

Sesilia Ngatunga na Charles Mbuluma ni wakazi wa Ruhuhu ambao wanasema watoto wao Wengi Wamekuwa wakikwama kuhitimu masomo kutokana na changamoto mbalimbali zikiwemo za kupata ujauzito na kukosa baadhi ya Vipindi wakati mito inapojaa maji wakati wa masika lakini sasa wataepukana na janga Hilo.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Deo Sanga na Halima Mamuya Mlezi wa CCM mkoa wa Njombe na mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa wamesema serikali itakwenda kukamilisha ujenzi wa shule ya Sekondari Ruhuhu ili watoto wapate Elimu kwa ukaribu na urahisi.
Screenshot 2025-02-04 154748.png
Screenshot 2025-02-04 154849.png
 
Back
Top Bottom