Katika sheria ya kazi nchini Tanzania...

Katika sheria ya kazi nchini Tanzania...

A Father

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2012
Posts
1,219
Reaction score
380
Je,katika sheria ya kazi nchini Tanzania kumetajwa muda maalum wa 'probation period' kabla ya kutia sahihi mkataba wa kazi? Kama 'ndio,' ni muda gani?

Nakushukuru kwa kupita hapa.
A Father.
 
Nadhani haijatajwa kabisa. Sikumbuki vizuri lakini.

Ila ni lazima kusaini mkataba wa kazi hata kama utaonyesha probation na kutoa vigezo. namaanisha kabla ya kuanza kazi lazma mkataba usainiwe kuwa tunakupa kazj hii na utakuwa probation kwa muda kadhaa. Kutegemeana na kazi unayopewa jnaweza kupewa probation hata ya mwaka mzima.

Pia mkataba unatakikana uwe na njia za kutoa feedback kama vigezo havifikiwi (mfano review ya mdomo, ikifuatiwa na review ya maandishi baada ya muda flani endapo haujafikia vigezo na kuambiwa unategemewa kufanya nini cha ziada). Hii itaondoa kuonewa.
 
Naomba msaada kwa hili je probabation time ukimaliza mwajiri anaweza kukuongezea? Na je sheria ya ajira na mahusiano kazini inamruhusu?
 
Probation period ni kuanzia miezi mitatu,na mwajiri aweza kuongeza muda wa probation mpaka kipindi kisichozidi miezi sita.
 
Mara nyingi ni miezi mitatu mpaka 6 kutegemea na mwajiri. Wapo waajiri wengine hawanaga habari ya probation if they are convinced of your capabilities. Hii mara nyingi ni common kwa poachers au head hunters.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom