Siku moja nikasema ngoja nimfuatilie asiyejulikana mmoja Nia nimkariri.
Akaja na gari moja tinted, ni kama walikuwa katika kunusa jambo Fulani,
Mahali pale palikuwa ni soko la kuuza samaki, dreva akashika breki, mlango ukafunguliwa, Sasa mimi nimeshanotice wale ni akina nani, nikakaza macho ili nimuone ashukaye ni nani, lengo ni kumkariri tu basi,
Gari iliposimama, mimi nikakaa angle nzuri ili akishuka nimuone, mlango ukafunguliwa kidogo, akausukuma, akatoa mguu, alivaa buti ya khaki ndefu, akawa kama anataka kushuka, nikakodoa macho yote kwamba nimemuweza Leo namuona, nikiwa naangalia bila hata kupepesa, mara mlango ukafungwa tena, gari ilikuwa silencer muda wote, nikasema hiki ni Nini! Gari ikasogea mbele kidogo, nani nikahama angle, kumbuka pale ni sokoni watu wengi.
Nikasogea mbele ,nikakaa kuangalia ikiwa atashuka, wakafika meter chache ya nilipokuwa, mlango ukafunguka tena ,mara hii akashuka ghafula chap akafunga mlango akaenda Kwa mama muuza samaki,
Kwani alinunua samaki Sasa? mara amulize swali, anashika mfukoni kama anatoa pesa, cha kushangaza hata hamuangalii muuza samaki, kichwa kinazunguka tu na macho huku na kule, mimi pia wakati huo sikutaka kuwaangalia, nikageuka kwingine,
Sasa alipogeuza shingo kumwangalia muuza samaki,si nikamwangalia, alivaa kofia, sura nikaiona tatizo ni kuiweka akilini, nilimwangalia zaidi ya mara tatu, Kila nikisave picha Kwa ubongo, inafutika, nilijaribu mara kadhaa bila mafanikio,
Wakati naendelea kujiuliza watu hawa wanatumia mbinu Gani kutokukaririka, nikaona ameshaingia kwanye gari haraka land cruiser tinted wakatembea.
Itoshe kusema mapichapicha ni mengi