Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Hello!
Rafiki yangu wa kazi, rafiki wa faida. Mimi na yeye sio marafiki kama nilivyoandika hapo juu ila tuko karibu kuliko hata hao mnaowaita marafiki.
Hatuongei jambo lolote isipokuwa issue ya fedha tu. Urafiki wetu ulikuwa kwenye mambo ya fedha pekee.
Nimeongea naye na kufanya biashara vizuri. Zimepita siku mbili naona simu yake akaniambia kuwa jana nikiwa kazini nilianguka ghafla na kuwahishwa hospital, nimefanyiwa vipimo vingi sana sina tatizo zaidi ya dalili tu za vidonda vya tumbo.
Akaendelea kuwa alikuwa hoi sana. Mwenyewe si mtu wa Rohoni nikamwambia hiyo ni michezo ya Uswahilini akasema ni kweli ni mambo ya wivu wanaona napata sana.
Haikupita wiki napata taarifa ya mshituko kuwa amefariki. Nimeumia sana, naona mkwamo wa kiuchumi mbele yangu. Lakini tajipanga upya. Pia nimeumia kwa dhuluma aliyofanyiwa.
Taarifa ya msiba nilipewa na mtu mmoja ambaye alimtuma dada mmoja aniombe namba, yule mtu namfahamu kidogo nimemwonea kama mara mbili tatu hivi. Nikampa namba akaniambia njoo hapa mara moja nikupe taarifa ya msiba. Nikaenda nikiwa na hofu nilihisi mwamba kafariki itakuwa maana jana nilipiga simu yake haijapokelewa na leo iligoma kabisa kuita.
Jamaa akaniambia Jamaa katangulia mbele za haki usihofu sasa biashara tufanye na Mimi. Wanadamu wabaya sana, siku unakufa tu watu wanakaba nafasi yako hawawazi familia yako, hawawazi safari yako kwa Mungu ikoje. Moja kwa moja nikamjua adui aliyemfanyia unyama rafiki yangu.
Kuwa makini na wanadamu, mtu yuko tayari akutupe kwenye shimo la futi elfu 10 ukaliwe na mijusi huko ili tu apate anachotaka bila kujali ukubwa wa kitu anachotaka.