Katika vita vya kibiashara hivi Trump anakusudia kupata nini ?

Katika vita vya kibiashara hivi Trump anakusudia kupata nini ?

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
10,509
Reaction score
16,734
Nimejaribu kujiunga na mtandao binafsi wa Trump wa Truth Social na sijafanikiwa.

Nilitaka nimuulize baadhi ya maswali anijibu na akishindwa nimpe elimu kidogo.


Swali langu ni hilo hapo juu.


Nilichotaka kumwambia Trump ana kwa ana ni kuwa anapigana na vita ambavyo atashindwa mchana kweupe.

Ni lazima atambue kuwa Dunia ni maumbile ya Mwenyezi Mungu ambaye kwa uadilifu wake amegawa fursa za kila namna eneo kwa eneo.


Madhumuni watu washirikiane na kubadilishana nyenzo walizonazo ili kila mmoja apate nafasi ya kumuabudu Mola wake kwa matayarisho ya maisha ya milele huko akhera.


Marekani ina vitu vingi lakini pia imenyimwa vitu vingi vyengine ambavyo lazima ivitafute kwa kubadilishana na ilivyonavyo.


Kutokuzingatia hilo na kulazimisha kila kitu kuwa nacho au kukipata bila gharama ni akili za kishetani na haziwezi kuleta faida wala ushindi wowote ule.

Katika nchi hata za jangwa basi fursa za kilimo zimegawanywa kiasi kwamba vitu wanavyohitaji kwa haraka kwa matumizi ya kila siku basi wanavipata huko huko.

Vichache ambavyo huhimili uharibifu kutokana na muda wameachiwa waviagize kutoka kwa wenzao kwa kubadilishana kibiashara na wenzao hao wa mbali.
 
 
Wachina hawafai. Na T-shirt wametengeneza na wanawauzia wamarekani.
Mchawi akikuloga we furahia TU.

 
Back
Top Bottom