Mganguzi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2022
- 1,604
- 3,715
Kama wewe unajua kwamba Mungu yupo! Hakikisha unatoa ZAKA. Fanya utani na masihara kwenye mambo yote lakini toa ZAKA! Babu yangu miaka Kumi iliyopita aliugua tb ambayo ilifanya apofuke macho! Hivyo akahudhuria kliniki na kuchoma sindano 120, lakini Bado hali yake haikubadilika ,naikumbuka siku Moja aliniita ni mwangalie mgongoni nikakuta anabanduka ngozi!
Akaniomba nianze kuitoa kwa kuibandua ,ilikuwa ni kazi ngumu ,unambundua ngozi mwili mzima na akiamka asubuhi ngozi unakuta ni kama jana hamkuibandua ,siku Moja yule babu alikata kauli ,watu wakakusanyika na kaburi likachimbwa ,alikuja askofu Mmoja hivi wa Moravian kutoka mission ya isoko Huko ileje mkoani songwe! Lakini kioja kilikuwa ni Kila wakiitoa maiti nje ili wakaizike inazinduka, anatikisa Mikono na kichwa ,wanaahirisha kuzika ,anaanza kupumua Tena kwa nguvu ,mnamrudisha ndani ,kaburi linafunikwa na mabati ,kesho mkiamka Tena mnakuta amekufa!
Kila wakijiandaa waanze ibada ya mazishi anazinduka,baada ya wiki Moja nakumbuka walikuja watumishi wengi kumuombea sana, siku ya saba alizinduka na kutamka maneno mazito kwamba nahitaji kutoa ZAKA, wakamwita askofu na mchungaji, wakaja kumsikiliza, walipoanza kumuuliza aliwajibu tena kwamba nataka kutoa ZAKA, bibi yetu akaruhusu atolewe ng'ombe kama zaka ya babu yetu, na akaomba akabidhiwe kamba ya Huyo ng'ombe kwa mkono wake akaikabidhi kwa askofu na wachungaji waliokuwepo ,walipoipokea na kuiombea na yeye akakata roho na hatimae akazikwa salama!
Hiki ni kisa kidogo lakini. Naamini sisi wengi hatuna elimu ya zaka ,mungu ndie akupae Kila kitu ,usione kama ni hasara kutoa zaka, hata kama Kuna watu watakubeza lakini toa ZAKA, kwa kadiri ya kipato chako ,hata kama hujawahi kuingia kanisani wewe agiza zaka Yako iende kanisani, au msikitini ama kwa mtumishi yeyote aliyekaribu Yako! Zaka inajitegemea na haihusiana na sadaka za kuwapa maskini na wahitaji Ile inaitwa ZAKA,
Kamwe usifanye mzaha kwenye kipengele cha zaka!
Uwe machinga, mpiga debe, mchoma chips, mama mboga ,mchimbaji ,mvuvi mkulima, mwanasiasa, shemasi, Mzee kanisa, doctor, msanii vyovyote ulivyo hakikisha unamtolea mungu zaka kila jumapili, kama huna muda wa kuhudhuria ibada nunua bahasha Yako ,Kila jumapili mwagize hata mtoto ataipeleka na itaombewa zaka Haina excuse, ni lazima.