Katika vitu ambavyo hutakiwi kusahau katika maisha yako ni kutoa Zaka, uwe Mkristo, Mpagani au Muislam

Katika vitu ambavyo hutakiwi kusahau katika maisha yako ni kutoa Zaka, uwe Mkristo, Mpagani au Muislam

Kusaidia masikini wenye uhitaji na wagonjwa au kumpa mchungaji hela yangu kwa jina la zaka kipi kina thamani mkuu?

Unaweza kumsaidia mtoto yatima ada ya shule au pesa ya matibabu akatibiwa akapona au unaweza kupeleka kanisani hiyo pesa kwenye bahasha kwa jina la zaka alafu jioni mchungaji akaenda kaunta kuagiza kvant au akachukulia demu hiyo hela kipi cha kupitishia zaka hapo mkuu
Zaka na Sadaka si ombi ni lazima
 
Hatuangalii imetumikaje tunachoangalia ni nia yako mtoaji juu ya zaka hiyo,kumbuka kabal hujatoa inene yaliyo mema.
 
Saidia kweli wasiojiweza....barikiwa sana
 
Kama wewe unajua kwamba mungu yupo! Hakikisha unatoa ZAKA! Fanya utani na masihara kwenye mambo yote lakini toa ZAKA! Babu yangu miaka Kumi iliyopita aliugua tb ambayo ilifanya apofuke macho! Hivyo akahudhuria kliniki na
ile zaka muhimu zaidi ni kuwatembelea na kuwapatia waginjwa, wazee , yatima na wahitaji mbalimbali wanaotuzunguka,
Hutanung'unika kwa mmiminiko wa faida za kiroho na za kimwili utakazojaaliwa na Allah.
 
Kwahiyo kila mkiitoa maiti nje inazinduka sio? Afrika kuna maujinga mengi sana!
 
Kama wewe unajua kwamba mungu yupo! Hakikisha unatoa ZAKA! Fanya utani na masihara kwenye mambo yote lakini toa ZAKA! Babu yangu miaka Kumi iliyopita aliugua tb ambayo ilifanya apofuke macho! Hivyo akahudhuria kliniki na kuchoma sindano 120 ,lakini Bado hali yake haikubadilika ,naikumbuka siku Moja aliniita ni mwangalie mgongoni nikakuta anabanduka ngozi ! Akaniomba nianze kuitoa kwa kuibandua ,ilikuwa ni kazi ngumu ,unambundua ngozi mwili mzima na akiamka asubuhi ngozi unakuta ni kama jana hamkuibandua ,siku Moja yule babu alikata kauli ,watu wakakusanyika na kaburi likachimbwa ,alikuja askofu Mmoja hivi wa Moravian kutoka mission ya isoko Huko ileje mkoani songwe! Lakini kioja kilikuwa ni Kila wakiitoa maiti nje ili wakaizike inazinduka, anatikisa Mikono na kichwa ,wanaahirisha kuzika ,anaanza kupumua Tena kwa nguvu ,mnamrudisha ndani ,kaburi linafunikwa na mabati ,kesho mkiamka Tena mnakuta amekufa! Kila wakijiandaa waanze ibada ya mazishi anazinduka,baada ya wiki Moja nakumbuka walikuja watumishi wengi kumuombea Sana ,siku ya Saba alizinduka na kutamka maneno mazito kwamba nahitaji kutoa ZAKA, wakamwita askofu na mchungaji ,wakaja kumsikiliza ,walipoanza kumuuliza aliwajibu Tena kwamba nataka kutoa ZAKA, bibi yetu akaruhusu atolewe ng'ombe kama zaka ya babu yetu, na akaomba akabidhiwe kamba ya Huyo ng'ombe kwa mkono wake akaikabidhi kwa askofu na wachungaji waliokuwepo ,walipoipokea na kuiombea na yeye akakata roho na hatimae akazikwa salama! Hiki ni kisa kidogo lakini. Naamini sisi wengi hatuna elimu ya zaka ,mungu ndie akupae Kila kitu ,usione kama ni hasara kutoa zaka ,hata kama Kuna watu watakubeza lakini toa ZAKA,kwa kadiri ya kipato chako ,hata kama hujawahi kuingia kanisani wewe agiza zaka Yako iende kanisani ,au msikitini ama kwa mtumishi yeyote aliyekaribu Yako! Zaka inajitegemea na haihusiana na sadaka za kuwapa maskini na wahitaji Ile inaitwa ZAKA,
Kamwe usifanye mzaha kwenye kipengele Cha zaka ! Uwe machinga ,mpiga debe ,mchoma chips ,mama mboga ,mchimbaji ,mvuvi mkulima ,mwanasiasa ,shemasi ,Mzee kanisa ,doctor ,msanii vyovyote ulivyo hakikisha unamtolea mungu ZaKa Kila jumapili ,Kama huna muda wa kuhudhuria ibada nunua bahasha Yako ,Kila jumapili mwagize hata mtoto ataipeleka na itaombewa zaka Haina excuse ! Ni lazima !
KAULI ZA MATAPELI WA KISOSHOLOJIA.
 
Attachments

Umeandika VYEMA sana mwanzoni katikati ila mwisho sasa unatuambia jumapili wakati wengine tunasali jumamosi, Wengine Ijumaa,Si ungemalizia tu kama ulivyoanza kwamba yeyote Kwa Imani yake atoe Zaka,Nakubaliana na wewe 100% kuwa Zaka ni jambo la muhimu sana kiimani na tulifanye liwe la kwanza kwani ni utii kwetu Kwa MUNGU wetu
Amin
 
Tusichanganye baina ya ZAKA na SADAKA. Ninavyofahamu ni kwamba:-

ZAKA ni sehemu ya KUMI au 10% ya mapato yako. Mfano kama umepata shilingi 1000/= ZAKA unayotakiwa kutoa ni shilingi 100/=

Kwa upande wa sadaka ni kiasi chochote cha pesa au mali ambacho moyo wako umeamua kutoa kwa Mungu. Sadaka haina kiwango maalumu. Lakini kumbuka: usitoe Sadaka kilema au Sadaka dhaifu. Chochote upandacho ndicho utakuwa. Ukitoa kwa ukarimu utakuwa kwa ukarimu. Ukipanda haba (uchoyo), utavuna kadiri ulivyopanda. Mfano wa kupanda haba ni huu: una kipato cha shilingi 1,000,000/ kwa mwezi halafu ukienda ibadani unatoa shilingi 500/=

Naishia hapo kwa leo. Muwe na jioni njema.
Zaka ni kwaajiri ya walawi, agano la kale, with new covenant zaka hakuna, Yesu alisisitiza kutoa ulichonacho na kuwasaidia wenye uhitaji. Haya mambo ya zaka yalikuwa specific for isralites
 
Hatuangalii imetumikaje tunachoangalia ni nia yako mtoaji juu ya zaka hiyo,kumbuka kabal hujatoa inene yaliyo mema.
Kumbuka Yesu alivyotoa mfano wa watu atakaosema " nilini ulituomba maji tukakunyima"? Yesu akawambia mnapo wasaidia watu mmenipa Mimi. Hivyo kutoa kwa wahitaji ni muhimu, pia kutoa kanisani au msikitini ni muhimu pia. Lakini wasiwatishe na kuwadanganya kuwa usipotoa mambo yako hayaendi sii kweli.
 
Back
Top Bottom