Katika ya Yanga fc inasemaje kuhusu kuwatoa viongozi?

changaule

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2020
Posts
6,039
Reaction score
10,151
Naomba kufahamishwa kuhusu katiba ya Yanga inasemaje ikiwa mashabiki hawana na imani na uongozi uliopo?

Mimi binafsi nimeona tatizo la Yanga ni Msola na magenge yake ndio wanairudisha nyuma timu ya Yanga. Kwanini?

1) amekuwa mtu aliyekosa mipango na mikakati sahihi kufikia kwenye target fulani. Kuna kipindi alikuwa anaunda unda mikamati tu kibao ambayo imeshindwa kufanikisha chochote kile cha maana. Ni kiongozi asiyejiamini na asiyejua nini afanye ili aifikishe Yanga kwenye hatua fulani.
2) kuanza upya kila mara.
Chini ya uongozi wa huyu Msola, Yanga wamevunja mabenchi pamoja na sajili mpya kila msimu. Hataki kuambiwa ukweli, ukifuatilia kilichomuondoa Zahera Mwinyi na Luc Eymael ni kuongea ukweli kwao.
Uongozi unakosa uvumilivu na kuwa wasikivu ili kuijenga timu, laiti kama kocha luc Eymael angeachwa basi muda huu Yanga wangekuwa hatua ya mbali kiuchezaji, kimbinu na kiufundi.

3) kuingilia majukumu
Kwavile anafani ya ukocha, anashindwa kuwaacha makocha waliopewa majukumu wakafanya kazi zao kwa jinsi wanavyoona wao inafaa badala yake anawaingilia majukumu yake

4) kucheza biti la mashabiki
Msola anakosa msimamo na kusimama katika nafasi yake na kusimamia kile anachokiamini na badala yake amekuwa ni mtu wa kufata mihemko ya mashabiki.
Mashabiki wamisema mbona fulani apangwi, wakisema sema tu utaona mechi inayofuata kapangwa ili mradi tu kuwasikiliza mashabiki
Tuliona namna Mwinyi Zahera, Lucy Eymael, Zlatko, na Kaze walivyoandamwa na mashabiki na kisha uongozi wakaufyata bila hata kufanya upembuzi. Yaani mashabiki ndio wanakuwa wafanya tathmini na kutoa hukumu kisha wao waigie tu.

5) msanii sana. Akiona mashabiki wana ng'aka sana anatafuta matukio ili kuwazima. Mfano alikuja na swala la mabadiliko kisha tuliiii anasubiri mashabiki waje juu ya mwenendo wa timu utaona anakuja na mwendelezo wa series yake ya mchakato wa mabadiliko.
Alikuja na swala la ujenzi wa uwanja saivi hakuna update yoyote mpaka itokee misuguano na mashabiki utaona analeta mwendelezo wa hiyo series yake uwanja.

6) kikwazo cha mabadiliko ya timu ya Yanga.
Tukiacha porojo, hakuna asiyejua kuwa mpira wa sasa unahitaji uwekezaji tena wakiwango cha pesa nyingi kuliko kiwango cha porojo. Lakini cha ajabu huyo mwenyekiti anataka kuuaminisha washabiki na wanachama kuwa timu inaweza kupata mafanikio kupitia uchangishaji eti kuwa ni mashabiki wengi ni mtaji mkubwa wa maendeleo.

Tusidanganyane kwa hilo mfumo mzuri wa timu kupata mafanikio ni kumpa timu muwekezaji/wawekezaji ili aendeshe ela. Hili litaifanya timu iendeshwe kisasa kwanzia kwenye uongozi mpaka kwenye benchi la ufundi kutakuwa na mipango, mikakati ili kufikia malengo. Lakini hilo la kutuaminisha kuwa eti timu ya wananchi na muwekezaji ni mwananchi ni uongo na lengo lako ni kuichelewesha Yanga kusimama kama ilivyosimama timu ya Simba.

Kuiga mazuri kwa jirani sio kitu kibaya, tumechelewa sana kuiga lakini bado muda upo kuiga kwa Simba vile ambavyo Mo ameichukua Simba na kisha kuiwezesha kucheza robo fainali mara mbili tokea alivyoichukua timu.

Yanga haitotokea ikapata mafanikio yoyote ya maana chini ya haya mapandikizi yaliyojuu ambayo ndio uongozi.

MSOLA KAMA UNA NIA YA DHATI JUU YA MAENDELEO YA YANGA BASI ANZA KWA KUJIUZURU UONGOZI KWASABABU MISIMU MITATU, YANGA HAKUNA WALICHOKIAMBULIA
 
Wewe siyo shabiki wa Yanga, wewe ni UTE....mnahangaika nini na Yanga[emoji706][emoji706]
 
Wewe siyo shabiki wa Yanga, wewe ni UTE....mnahangaika nini na Yanga[emoji706][emoji706]
Akili za mashabiki kama nyie ndio mtaji mkubwa kwa viongozi. Mtu akizungumza ukweli anakuwa sio mshabiki wa Yanga
 
Akili za mashabiki kama nyie ndio mtaji mkubwa kwa viongozi. Mtu akizungumza ukweli anakuwa sio mshabiki wa Yanga
Umeanzisha thread ya kichochez, ambayo mazingira yake yanaonesha kuwa wewe ni ama ni mmoja wa maadui wa aman ya Yanga au ni adui wa viongozi wa Yanga.

Wewe viongozi wameshasema wapo kwenye kipindi cha kufanya mabadiliko tupate proper management, unakuja kubwabwaja hapa kuuponda! Sasa kama timu haipafom na 70% ya wachezaji wame flop unaulaum uongozi kwa lipi! Underperform kwenye timu ni kitu cha kawaida kama kweli unaufaham mpira wa miguu.
 
Sasa wachezaji wameflop wamesajiliwa chini ya uongozi upi? Kwanini kila msimu timu ianze na upya?
 
Sasa wachezaji wameflop wamesajiliwa chini ya uongozi upi? Kwanini kila msimu timu ianze na upya?
Me siyo mtaalamu wala mwalimu wa mpira ila kwa upumbavu na ukilaza wangu najua sababu ya kuflop kwa mchezaji main ni psychological na siyo viongozi yan!
 
Me siyo mtaalamu wala mwalimu wa mpira ila kwa upumbavu na ukilaza wangu najua sababu ya kuflop kwa mchezaji main ni psychological na siyo viongozi yan!
Naomba nipe ufafanuzi nivipi kila mchezaji anayesajiliwa ana flop kwasababu ya psychological?
 
Me siyo mtaalamu wala mwalimu wa mpira ila kwa upumbavu na ukilaza wangu najua sababu ya kuflop kwa mchezaji main ni psychological na siyo viongozi yan!
Naomba nifahamishe wajibu wa viongozi ni upi halafu niambie ni vipi wao hawahusiki na timu inapokuwa na matokeo mabaya
 
Naomba nipe ufafanuzi nivipi kila mchezaji anayesajiliwa ana flop kwasababu ya psychological?
Nakupa sababu chache tu ila pia siyo wote walioflop.
Sababu kubwa ya wachezaji kuflopYanga ni mazingira,
Yanga ndiyo mabingwa kwa kihistoria wa ligi kuu,
Yanga ndiyo timu kongwe Africa mashariki,
Yanga miongon mwa timu chache Africa zilizohusika kwenye mchango wa Uhuru wako na Taifa lako dhidi ya wakolon,
Yanga ndiyo timu yenye mashabiki wengi Tanzania kama si Africa.

Kwa mazingira hayo hapo juu, chanzo kikubwa cha kuflop kwa wachezaji ni presha ya ukubwa wa timu na fans base na siyo Viongozi. Kwa ukubwa wa Yanga ilitakiwa timu iwe na mwanasaikolojia kwa ajili ya counseling.
 

Kwahiyo kipindi ambacho Yanga ilikuwa inachukua ubingwa mfululizo je Yanga ilikuwa na mwanasaikolojia? Je ukubwa wa yanga haukuwepo?
 
Kwahiyo kipindi ambacho Yanga ilikuwa inachukua ubingwa mfululizo je Yanga ilikuwa na mwanasaikolojia? Je ukubwa wa yanga haukuwepo?
Wewe jamaa, hebu shusha hapa Elim yako, nsije nkawa na argue na Msukuma type[emoji42][emoji42]!

Soma posts zangu uelewe contents ndiyo ujibu mtan!
 
Wewe jamaa, hebu shusha hapa Elim yako, nsije nkawa na argue na Msukuma type[emoji42][emoji42]!

Soma posts zangu uelewe contents ndiyo ujibu mtan!
Sina elimu yoyote. Wewe unakataa kuwa viongozi hawahusiki kwa matokeo mabaya nimekuomba unipe majukumu ya viongozi ni yapi ili tuone kama hawahusiki na timu kufanya vibaya. Umesema kuwa wachezaji wanaflop kutokana na ukubwa wa Yanga kuwaathiri kisaikolojia. Sasa ndio maana nimekuuliza kipindi cha nyuma je Yanga walikuwa na mtu wa saikolojia ili kuwafanya wafanye vyema mpaka wakachukua ubingwa mfululizo? Au huo ukubwa wa yanga haukuwepo kwa kipindi hiko?
 
Mtan timu zetu hazijafikia huko kuanza kuwalaum viongoz kisa mchezaji au wachezaji kuflop, mfano huyo Suppong, Fiston wametoka huko wakiwa wafungaji, wachezaji bora kwenye vilabu vyao, kuwalaum viongozi ni kuwaonea, timu zetu za kiafrica haina resources za kutosha za ku protect na ku develop wachezaji mentality & physically sababu ya pesa, wanachama na mashabiki tunakesha tunaponda viongozi humu, je tunaichangia timu yetu kimawazo na kifedha! Viongozi wa Yanga wanajitahid kwa wanaloliweza, na hiki kipindi cha COVID kupata investors aina ya GSM na MO umshukuru sana Mungu!
 
Kipind cha usajil kila shabik na watu wa yanga walikua pamoja na gsm na sio vipngoz ,tena kuna kipind hawa akina msola walikua kama wanaitaj na wao wafanye kaz yao lkn gsm wakaona wanaingiliwa wakatishia kujitoa ikawa balaa hakuna ata shabik au mwanachama aliekua upande wa akina msola ata kipind ambacho yanga inafanya vzur sifa zote ni za akina gsm,yanga ikiyumba ndio shutuma kwa akina msola tuwe wakwel tu hii yanga kama inakosa ubingwa wa kulaumiwa gsm na kwa sababu wao ndio kila ktu sio utengenezaj na uuzaj tu jez wao timu ndio wanasaut kuliko hao akina msola ata mashabik weng ni gsm msola ataongea nn aeleweke na shabik au watu wa yanga zaid ya inginia na nugaz.
 
Umetaja nguvu ya pesa kwenye mchezo wa mpira wa miguu. Upo sahihi sana juu ya hilo na ndio maana kwenye uzi wangu nilipinga kauli iliyokuwa inaamasishwa na viongozi kwamba timu ya wananchi, wawekezaji ni wananchi. Ili kupata mafanikio kwenye mpira wa miguu ni kuwapa timu wawekezaji.

Jambo la pili ni kujenga timu, hauwezi kujenga timu kwa kuvunja vunja mabenchi ya ufundi kila msimu ama nusu ya misimu. Na pia kila kila msimu unaacha wachezaji 5+ na kusajili wachezaji wengine wapya
 
Na ndiyo maana GSM wameiona hiyo weaknesses sasa wanafadhili mabadiliko ili pawe na proper management timu iendeshwe ki professional.
 
Timu ambazo Simba SC inaweza kucheza nazo fainali ya Klabu Bingwa Dunia mwaka huu
1.Man City
2.Chelsea
3.Real Madrid
4.PSG"
 
Yanga ndiyo mabingwa kwa kihistoria wa ligi kuu. Yanga ndiyo timu kongwe Africa mashariki, Yanga miongon mwa timu chache Africa zilizohusika kwenye mchango wa Uhuru wako na Taifa lako dhidi ya wakolon,
Timu inasifiwa kwa hali iliyopo sasa, na si kwa historia. Watu wanaenda uwanjani kushangilia timu zinazocheza, sio zilizocheza!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…