changaule
JF-Expert Member
- Jan 10, 2020
- 6,039
- 10,151
Naomba kufahamishwa kuhusu katiba ya Yanga inasemaje ikiwa mashabiki hawana na imani na uongozi uliopo?
Mimi binafsi nimeona tatizo la Yanga ni Msola na magenge yake ndio wanairudisha nyuma timu ya Yanga. Kwanini?
1) amekuwa mtu aliyekosa mipango na mikakati sahihi kufikia kwenye target fulani. Kuna kipindi alikuwa anaunda unda mikamati tu kibao ambayo imeshindwa kufanikisha chochote kile cha maana. Ni kiongozi asiyejiamini na asiyejua nini afanye ili aifikishe Yanga kwenye hatua fulani.
2) kuanza upya kila mara.
Chini ya uongozi wa huyu Msola, Yanga wamevunja mabenchi pamoja na sajili mpya kila msimu. Hataki kuambiwa ukweli, ukifuatilia kilichomuondoa Zahera Mwinyi na Luc Eymael ni kuongea ukweli kwao.
Uongozi unakosa uvumilivu na kuwa wasikivu ili kuijenga timu, laiti kama kocha luc Eymael angeachwa basi muda huu Yanga wangekuwa hatua ya mbali kiuchezaji, kimbinu na kiufundi.
3) kuingilia majukumu
Kwavile anafani ya ukocha, anashindwa kuwaacha makocha waliopewa majukumu wakafanya kazi zao kwa jinsi wanavyoona wao inafaa badala yake anawaingilia majukumu yake
4) kucheza biti la mashabiki
Msola anakosa msimamo na kusimama katika nafasi yake na kusimamia kile anachokiamini na badala yake amekuwa ni mtu wa kufata mihemko ya mashabiki.
Mashabiki wamisema mbona fulani apangwi, wakisema sema tu utaona mechi inayofuata kapangwa ili mradi tu kuwasikiliza mashabiki
Tuliona namna Mwinyi Zahera, Lucy Eymael, Zlatko, na Kaze walivyoandamwa na mashabiki na kisha uongozi wakaufyata bila hata kufanya upembuzi. Yaani mashabiki ndio wanakuwa wafanya tathmini na kutoa hukumu kisha wao waigie tu.
5) msanii sana. Akiona mashabiki wana ng'aka sana anatafuta matukio ili kuwazima. Mfano alikuja na swala la mabadiliko kisha tuliiii anasubiri mashabiki waje juu ya mwenendo wa timu utaona anakuja na mwendelezo wa series yake ya mchakato wa mabadiliko.
Alikuja na swala la ujenzi wa uwanja saivi hakuna update yoyote mpaka itokee misuguano na mashabiki utaona analeta mwendelezo wa hiyo series yake uwanja.
6) kikwazo cha mabadiliko ya timu ya Yanga.
Tukiacha porojo, hakuna asiyejua kuwa mpira wa sasa unahitaji uwekezaji tena wakiwango cha pesa nyingi kuliko kiwango cha porojo. Lakini cha ajabu huyo mwenyekiti anataka kuuaminisha washabiki na wanachama kuwa timu inaweza kupata mafanikio kupitia uchangishaji eti kuwa ni mashabiki wengi ni mtaji mkubwa wa maendeleo.
Tusidanganyane kwa hilo mfumo mzuri wa timu kupata mafanikio ni kumpa timu muwekezaji/wawekezaji ili aendeshe ela. Hili litaifanya timu iendeshwe kisasa kwanzia kwenye uongozi mpaka kwenye benchi la ufundi kutakuwa na mipango, mikakati ili kufikia malengo. Lakini hilo la kutuaminisha kuwa eti timu ya wananchi na muwekezaji ni mwananchi ni uongo na lengo lako ni kuichelewesha Yanga kusimama kama ilivyosimama timu ya Simba.
Kuiga mazuri kwa jirani sio kitu kibaya, tumechelewa sana kuiga lakini bado muda upo kuiga kwa Simba vile ambavyo Mo ameichukua Simba na kisha kuiwezesha kucheza robo fainali mara mbili tokea alivyoichukua timu.
Yanga haitotokea ikapata mafanikio yoyote ya maana chini ya haya mapandikizi yaliyojuu ambayo ndio uongozi.
MSOLA KAMA UNA NIA YA DHATI JUU YA MAENDELEO YA YANGA BASI ANZA KWA KUJIUZURU UONGOZI KWASABABU MISIMU MITATU, YANGA HAKUNA WALICHOKIAMBULIA