G-Mdadisi
Senior Member
- Feb 15, 2018
- 165
- 100
KATORO, Geita. Kijiji pekee nchini kwasasa chenye hadhi ya kuitwa MJI lakini bado kinatambulika kama Kijiji sawa sawa na kijiji cha KASATO kule Biharamulo, ama Kiuyu Mbuyuni kule Micheweni, Pemba Zanzibar.
UKipata fursa ya kufika KATORO. Hapa kuna
BENKI karibu zote uzijuazo
MAJI ya kutosha
UMEME wa uhakika
MIUNDOMBINU ya Barabara bora hadi mitaani kuzidi hata meneo mengi yenye hadhi ya mji.
KATORO Ndilo lango la wafanyabiashara wa Nguo, urembo n.k (MACHINGA), pikipiki na bidhaa mbapimbali kutoka mikoa ya Kagera, Mwanza,Shinyanga, Simiyu, Dodoma, Tabora, Kigoma, Singida, hadi nchini UGANDA.
Cha kuvutia zaidi ni kwamba KATORO ni miongoni mwa maeneo salama, na yenye maisha rafiki kabisa kwa kila mtanzania kumudu kuishi kulingana na uwezo wa kipato chake. Hapa bidhaa ni bei ya kawaida sana ukilinganisha na maeneo mengine (kama wewe ni mtembeaji)
Licha ya ukubwa wa eneo hili kibiashara na kimaendeleo lakini bado #KATORO kiserikali inatambulika kwa hadhi ya KIJIJI ikiongozwa chini ya serikali ya KIJIJI na KATA.
Mpango wa kuzaliwa kwa mkoa mpya wa CHATO huenda ukaja kuzaa mabadiliko ya hadhi ya eneo hili la Katoro na kupata fursa ya kupanda hadhi kwani hapa ni moja ya maeneo ambayo bado mamlaka hazijayatendea haki kabisa na yana kila sababu ya kuitwa mji kutokana na kasi ya maendeleo iliyopo.
Kama hili la kuundwa kwa mkoa mpya wa #Chato litafanikiwa, sehemu ya kwanza na hazina kimkakati ni eneo hili kwani hapa ndipo pesa zinatengenezwa. Linahitaji kuangaliwa na kupewa hadhi yake.
Wasalaam
#GMdadisi