Katuga alijaribu kuielekeza Mahakama kutoa adhabu kinyume cha sheria

Katuga alijaribu kuielekeza Mahakama kutoa adhabu kinyume cha sheria

Consigliere

Platinum Member
Joined
Sep 9, 2010
Posts
12,901
Reaction score
27,423
Katika final submission, Katuga alileta hoja ambayo kwa mtazamo wangu ndiyo sehemu yenye utata mkubwa zaidi kwenye suala la adhabu. Alidai kwamba Section 39(2)(d) inatumia maneno “shall be liable”, na kwa hiyo Mahakama ina discretion ya kutoa adhabu kuanzia kifungo cha kawaida hadi death penalty. Akafika mbali zaidi kusema kwamba punishment inaweza “range from zero to hanging.” Hii ndiyo hoja aliyoiwasilisha kama msingi wa kuomba Mahakama ione kwamba conviction ya treason haimaanishi lazima Lissu anyongwe.

Tatizo ni kwamba ukienda kwenye official Penal Code R.E. 2023, wording ya Section 39(2) ni tofauti kabisa na hiyo description. Kifungu kinasema mtu anayefanya matendo yaliyoainishwa, ikiwemo chini ya paragraph (d), “commits treason and on conviction, shall be sentenced to death.” Hakisemi “shall be liable to death.” Kwa hiyo, kama Katuga alijenga hoja yake ya sentencing juu ya maneno “shall be liable”, swali la msingi ni: anatumia version ipi ya Section 39(2)(d), na kwa nini Mahakama ikubali interpretation hiyo wakati official R.E. 2023 yenyewe inatumia maneno “shall be sentenced to death”?

Na hapa ndipo Hatibu Gandhi v Republic inakuwa muhimu. Katika Gandhi, Court of Appeal ilisema kwamba proof ya overt act peke yake haitoshi, lazima kuwe na proof ya appropriate intention na allegiance. Kuhusu sentence, Court ilisema maximum penalty ya treason ilikuwa death, lakini life imprisonment iliyokuwa imetolewa kwa washtakiwa hao ikaendelea kusimama. Hivyo Katuga alikuwa na kazi mbili tofauti: kwanza, kuishawishi Court kuhusu guilt chini ya s.39(2)(d), na pili, kuishawishi Court kuhusu maana na effect ya statutory punishment. Kwenye sehemu ya pili, hoja yake ya “shall be liable” inapaswa kuchunguzwa kwa umakini mkubwa kwa sababu wording ya official R.E. 2023 haijasema hivyo. Hapo ndipo ninapoona kuna hatari ya Court kupewa interpretation ya adhabu ambayo haianzi na maneno halisi ya kifungu chenyewe.
 
Kama tulimpumzisha Kihiyo na kuacha kutumia neno 'Kihiyo' kumaanisha mtu mwenye elimu magumashi na muongo muongo, kwa sasa neno 'Katuga' liwe ndiyo neno lenye kumaanisha tapeli wa sheria na mtu muongo muongo anayedanganya hadi majaji
 
Kama tulimpumzisha Kihiyo na kuacha kutumia neno 'Kihiyo' kumaanisha mtu mwenye elimu magumashi na muongo muongo, kwa sasa neno 'Katuga' liwe ndiyo neno lenye kumaanisha tapeli wa sheria na mtu muongo muongo anayedanganya hadi majaji
Hii imepitishwa
 
Katuga ndio anabeba lawama zote na furushi la ujinga/mavi lote. Wenzake wamekaa kimya, CDF na IGP wamejificha mafichoni, mama yao ako Edan
 
Screenshot_20260930_152012_My Files.jpg
 
Back
Top Bottom