Cannabis
JF-Expert Member
- Jan 20, 2014
- 11,557
- 33,535
Katuni maarufu ya Scooby-Doo ambayo imekuwa ikionyeshwa katika chaneli mbali mbali kama Cartoon Network, imemtambulisha mmoja wapo wa wahusika kama msagaji (lesbian).
Mhusika huyo anayeitwa Velma ameonyeshwa katika toleo jipya la katuni hiyo kama mwanamke anayevutiwa kimapenzi na mwanamke mwingine.
Hali hiyo imepelekea mgongano wa mawazo katika mitandao ya kijamii nchini Marekani, ambapo baadhi ya watu wamesema hakukuwa na ulazima wa kuweka maudhui hayo katika katuni ya watoto.
Kutokana na maamuzi hayo mtandao wa Google umeonekana kuunga mkono maamuzi hayo ambapo wameweka rangi nyingi za upinde wa mvua pale mtu anavyotafuta neno "Velma" katika mtandao huo kama inavyoonekana kwenye picha.
Hali hii inazidi kuonyesha uhitaji wa ongezeko la umakini wa wazazi kuhusiana na maudhui ambayo watoto hujifunza kutoka kwenye katuni ambazo zimekuwa zikitazamwa kwa miaka mingi hapa nchini Tanzania.