jamaa na ma bandeji miguu yote mpk mikononi.hata kuupiga huo mpira ni tabu.
movie imekua tam balaa
Hiyo sio be penalty, ni set piece
Chadema wako hoi...uwezekano wa kufunga hiyo penati ni mdogo sana.
Msanii Kipanya ameendelea kuzikonga nyoyo za wapenzi wa michoro hiyo hasa kipindi hiki ambacho ccm ipo kwenye sintofahamu ya kiuongozi.
Tafadhali tazameni hiyo picha chini hapoView attachment 1158779
JF ni sehem ya Great Thinkers.. wewe si mmoja wetu sijui uliingiaje humu aiseeUpuuzi mtupu,ccm haiwezi toka madarakani kwa kanituni za kipuuzi kama hizi,nendeni kwa wananchi mkauze Sera wananchi wawapime,unadhani tabiri uchwara za kipanya zina nafasi yotote katika kuingoa ccm?
Mpigaji asije akapaisha jamani!
Jamaa katoka fb huyoJF ni sehem ya Great Thinkers.. wewe si mmoja wetu sijui uliingiaje humu aisee
Hapa anamanisha kuwa wakati wa MABEKI WA CCM WANAFARAKANA ni muda mzuri kwa mjeruhiwa CHADEMA kupiga shoot kuelekea golini.
Cartoon hii ina maana nyingi. Kipanya anaweza kuwa anamaanisha kwamba baada ya upinzani kuvunjwavunjwa miguu na kupata makovu ya kutosha, CCM ya sasa ya Jiwe imepata kiburi na inaweza kuachia goli wazi ikiamini hawa jamaa hawana uwezo wa kupiga shuti kali la kuingia nyavuni. Unaweza kuhusisha hii na kitendo cha Jiwe cha kutumbua wale wooote waliofanikisha goli la mkono. Anadhani hawahitaji tena
Mbona kama wameamua kulikimbia goli na hapo mwana cdm anajipanga kupiga penati wakati lango lipo tupu?
Ukiona mchoro una majibu rahisi ya kuattack upande mmoja basi hapo kazi ya sanaa imefeli
Mpiga penalty anaweza kushindwa kupiga hiyo penalty au hata akipiga anaweza Kupiga nje au mpira usifike kabisa golini pamoja na goli kuwa wazi..
Upinzani wanahitaji kuwa majasiri kidogo tu kuiyumbisha CCM wakati huu.. Bila ujasiri hawataweza kuitoa CCM..
Mpiga penalty anaweza hata kumwomba beki wa timu pinzani aje apige km ilivyotokea 2015. Halafu beki akapiga nje!
Hii siioni kama ni penalty. Bali ni mpira wa adhabu uliotengwa jirani na lango la timu (yenye jezi Kijani na Njano), ambayo mabeki wake pamoja na golikipa walipaswa kujipanga vizuri ili kuzuia mpira utakaopigwa. Ingelikuwa ni penalty, bas tungemshuhudia mpigaji na golikipa pekee pichani. Wengine wangekuwa kando kidgo. Kwahiyo kwa kifupi walinzi wa timu ya Kijani na Njano wameshindwa kujipanga, na pia upande mwingine sio ajabu mpigaji akishindwa kutumia madhaifu ya safu hiyo ya ulinzi kutokana na yeye mwenyewe kutokuwa physically fit. Si ajabu akalenga goli, ila shuti likashindwa kufika/ kuvuka mstari wa goli.
Mchoro hauja attack upande wowote ila unahitaji akili kubwa kuupambanua....
Acha picha iongee π π π