Kauli 10 za walimu darasani

''siyo wote waniitao bwana bwana watauona ufalme wa mungu" hiyo ilikuwa ni kauli ya mwl mmoja wa basic mathematics kigoma sec!

alikuwa anakuja na mathematical tables(four figures?) za kutosha darasa zima lakini anazigawa kwa baadhi ya wanafunzi wanaojua hesabu tu.

Zinazobaki anaziweka mezani! hilo lilikuwa jibu la mwanafunzi aliyehoji ni kwa nini wengine hawajagawiwa wakati zimebaki za kutosha darasa zima!?
 

Ha ha ha nimecheka hadi basi daaah nikaunganisha na vichekesho vingine yan ndio nikazidisha kicheko.
 
You just crame, you will understand leter!
Kwanza huwa haitoki kwenye mtihani

Hiyo kauli pia alikuwa anaitoa Ass. Lectrr.. mmoja hivi Mbeya University of Sc and Tech. (MUST) wa idara ya Mechanical
 
1) Hata nkusomesheni vipi, yanaingia upande wa kulia na yanatoka upande wa kushoto

2) mkifika kwenu mabuku mnayatupa tu

3) wazazi wenu wamechoka kukuleeni ndo mkaletwa huku

4) ukitoroka namwita mzazi wako

5) nyinyi ndo mtakua viongozi kesho

6) asiyefanya kazi ya darasani atantambua mimi nani
 
MOSSAD II

hahahaha! mkuu, nimecheka sana. inaonekana huyo mwalimu alikuwa BANDITU wa kufa mtu.
 
Last edited by a moderator:
Time is over, stop writing and put your PENS down!

Hayo yalikuwa maneno kutoka kwa ivigilator (supervisor), kila muda wa mtihani unapoisha. Ilikuwa mwa 1990 wakati tunafanya mitihani ya darasa la nane (KCPE).

Mitihani yote ni multiple choice na huandikwa kwa penseli ya HB na kuwa marked kwa kutumia mfumo wa OMR lakini msimamizi alikuwa amekariri sana neno PEN badala ya PENCIL.
 
mna miandiko mibaya kama bata anaparua

kuna mwalimu m1 primary alikuwa napenda kusema

‘ona yalivyo nyoronyoro kama utumbo wa bata'.

kuna siku nilienda home nikakutana naye nikajikuta nacheka tuu!

ikanibidi nimwachie buku 20 akanywe soda.
 
enzi hizo hakuna mabegiya kuwekea daftari, tunazitumbikiza mgongoni, ukifika home usipokumbuka kuzitoa mgongoni asubuhi unaamka nazo, unaingia clas tena, tumetoka mbali sana.
 
Yani mmeharibu nauli zenu kuja hapa Ndanda ili mfaulu PCB au PGM? bora hamia HKL au HGK la sivo mtarudi kwenu kama mlivokuja,hasa wewe unaenikodolea macho (akaninyoshea kidole).

Dah! mkuu umenikumbsha mbali sana nilikuwa ndanda pgm.
 
Ww kibwengo unashida gannniiii........daaa namkumbuka ticha wetu wa hesabu miaka 1993 yey alikua akiingia darasan wanafunzi wote wanasinzia sasa kauli yake ndio ilikua hiyo......hadi kicheko nkimkumbuka aiseeee
 
1.UNIVERSITY hatuend kwa gari 'ok!' 2. mwaka huu tumeamua tutoe ZERO," hii ilikuwa MAKITA,Mbinga-Ruvuma 2014/15.
 
1) AKILI YAKO HAINA AKILI/AKILI YAKO IMEZUBAA.
primary/kisw. Teacher.

2) NANGA MKUBWA WE!
primary/sci. Teacher

3) NYANYUA NYUNGU MTOTO.
(meaning; nyanyua matako juu ili akuchape vizuri unapokuwa umelala chini kwaajili ya kuadhibiwa)

4) NTAKUNYONYA DAMU MTOTO!
-Olevel/Cleanliness Teacher.

5) KWA UPUMBAVU WAKO HUO HUO RUDI NYUMBANI KATULETEE MZAZI WAKO.
H/Master Olevel.
 
SIO BABA ZENU NA MAMA ZENU WASIOJUA HATA TAKO LA "a" LINAKAAJE. nilikua nachoka sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…