Kauli 6 alizowahi kutoa Mzee wa Upako ambazo zilileta taharuki nchi, anajua kucheza na muda kufanya atrendi

Kauli 6 alizowahi kutoa Mzee wa Upako ambazo zilileta taharuki nchi, anajua kucheza na muda kufanya atrendi

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Habari za asubuhi wakuu.

photo_5969614786499035943_x.jpg

Siku ya jana, Mzee Wa Upako yaani Mchungaji Anthony Lusekelo alitengeneza headlines nchini kufuatia interview alyofanya na Jambo TV Online ambapo alizungumzia upepo wa kisiasa ulivyo nchini ikiwemo ishu za utekaji, ukosoaji unaendelea dhidi ya Rais Samia na mengineyo.

Lakini hii si mara ya kwanza kwa Mzee Wa Upako kutoa kauli ambazo zimeshtua na kutengeneza headlines Tanzania.

Tofauti na viongozi wengine wa kiimani ambao mara nyingi wamekuwa low profile kuzungumzia ongoing issues, Lusekelo amekuwa wa tofauti.

Here is how many times, mchungaji huyu ametengeneza headlines na kauli zake:

1. Nampenda Diamond, Ali Kiba Ana Kiburi

Mei 2018, Mzee Lusekelo aliingia kwenye headlines baada ya kusema kuwa anampenda Diamond zaidi kuliko Ali Kiba kwa sababu Diamond anaonekana kuwa Mnyenyekevu zaidi kuliko Ali Kiba

Diamond Ali Kiba.jpg

Pitia: Mzee wa Upako: Nampenda Diamond kwa sababu ni mnyenyekevu, simpendi Alikiba ni kiburi

2. Walionichafua Watakufa

Hii aliisema Desemba 2016 ambapo akiwa anaongea kwenye mahubiri yake ambapo alisema kuwa kila mwandishi wa habari aliyemuandika vibaya atakufa.

Soma Pia<<< Mzee wa Upako: Wote Walionichafua Watakufa Mwakani, Wasipokufa Nitaanza Kuuza Gongo

3. Unakujaje Kanisani Bila Sadaka?

Kwa wale wote ambao mnaenda kanisani bila kutoa sadaka, Lusekelo alitupa jiwe gizani July 2024 akiwa kwenye interview pale Wasafi FM kwa kuhoji wazi wazi kuwa Unakujaje Kanisani Bila Sadaka?

Swali likawa ni, je kama hauna sadaka hautakiwi kwenda kanisani?



4. Ishu Ya Tozo

Septemba 2022, Mchungaji Anthony Lusekelo alileta mjadala mkubwa mitandaoni baada ya kutetea tozo zilizoletwa na uongozi wa Rais Samia kwenye mitandao.

Katika kipindi ambacho Watanzania walikuwa wanalalamika kuhusu tozo, Lusekelo alijitokeza hadharani na kutetea tozo kwa kudokeza kuwa zilianza tangu kipindi cha torati.

Pitia<<< Mzee wa upako: Nchi itajengwa na wananchi wenyewe

5. Wagombea Urais Lazima Wawe Na Cheti Cha JKT

Mwaka 2022, Mzee Wa Upako aliishauri Tume Ya Uchaguzi yaani NEC kuweka kuhitimu JKT kama kigezo cha mwanasiasa kuruhusiwa kugombea Urais.

Pitia>>> Mzee wa Upako ataka wagombea Urais kuwa na cheti JKT

Hizi ni baadhi tu ya kauli za Mzee Wa Upako, kama unakumbuka nyingine tupia hapo chini.
 
Usihukumu usije ukahukumiwa maana kipimo kile kile unachopimia wenzako na wewe ndicho utakachopimiwa tena kwa kujazwa na kushindiliwa na kusukwasukwa
 
Back
Top Bottom