Kauli hii ya Kardinal Pengo,inatukumbusha "upande wa pili" wa Kanisa Katoliki

Kauli hii ya Kardinal Pengo,inatukumbusha "upande wa pili" wa Kanisa Katoliki

Hivi mtuhumiwa anajipeleka polisi ajieleze makosa yake?

Kinawashinda nini kuanisha uongo?

Barua za serikali hazinihusu.

Kama umetumwa kawaambie huu upuuzi wenu unafahamika na tupo wengi hatufurahii licha ya kwamba hamlisaidii taifa.
Looks like trying to make logical argument with you my efforts will be futile. Unaendeshwa na hisia sio uhalisia.
 
Mtuhumiwa ni serikali kwamba imetoa maagizo hayo ya upendeleo kama unavyotaka kutuaminisha.
Mtoa tuhuma dhidi ya serikali ni wewe ambae tunakuomba lete ushahidi kuthibitisha tuhuma zako.
Nithibitishie wewe ni mahakama na una shauri gani mahakamani ili niwe shahidi wako.

Tupo kwenye mjadala kama hizi unaona ni tuhuma zipeleke kunakostahili zifanyiwe kazi.
 
Asili ya kanisa katiliki si kutetea wanyonge, bali kujilimbikizia mali na maeneo makubwa ya vitega uchumi.
 
Wakati mwingine nikikumbuka kauli za Gwajima kwa Kardnal Pengo Nina pata Ukweli halisi juu ya kufikiri kwa kiongozi wetu.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Thanks again I rate this thread #1 for 2016.

Hongera kuliita jembe ni jembe na siyo rato.

Nikutonye, unakumbuka mara baada ya awamu hii kuingia madarakani kulipigwa marufuku kufanyia seminar makongamano au mikutano kwenye kumbi au hoteli binafsi.

Basi yalihamishiwa yote kwenye kumbi za Kanisa Katoliki TEC au Msimbazi kwa DSM na mtukufu Mtakatifu alibariki. Kwa hiyo Pengo anasema kweli kuwa wamevuka malengo kwa monopoly hiyo.
Kumbe ndo maana tuna wakengeufu wengi sana hata CDM waliingizwa mkenge kwenye UKUTA mwanzo ati viongozi wa dini wanaongea na mkulu kumbe viongozi wenyewe ilikuwa poza joto wala haikuwepo kuongea na mkulu wala nini mpaka Leo hakuna report kama waliingea au lah.
 
Wakati mwingine nikikumbuka kauli za Gwajima kwa Kardnal Pengo Nina pata Ukweli halisi juu ya kufikiri kwa kiongozi wetu.
Tumuombee Mwandhama;ili akae ktk kile ambacho wanyonge na masikini wa Kanisa Katoliki wanakionja ktk dhiki na taabu ya maisha yao ya kila siku
 
View attachment 451101

Watu wametweta,wamekasirika na wengine wamefura kwa maneno mazitomazito kwa kauli ya Mwadhama P. Kardinal Pengo.Yeye Pengo kama baba wa kiroho na kiongozi wa waumini wa kanisa katoliki jimbo la Dsm hakubaliani na kauli kuwa sasa "Hela imekuwa adimu mifukoni" na sasa "maisha yamekuwa magumu tilatila".

Mbele ya mimbari ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph,baba mlishi wa Yesu Kristo,fundi selemala wa Nazareth,Kardinali Pengo anapiga msumari wa moto ktk mioyo ya waumini wake.Waumini walioanza kukata tamaa na kutegemea maneno ya faraja toka kwa baba wa kiroho,wanakutana na kauli ngumungumu zinazowaumiza.

Pengine wale "waumini rasharasha" wameanza kunung'unika,wanasononeka kwa taharuki,wanajiuliza,kama huyu tuliomtegemea atusemee,mbona anatukatisha tamaa na kutokuwa upande wetu?Inastua...lkn inakatisha tamaa,pale ambapo wengi tunaongea lugha moja ya "hela imekuwa adimu",mwingine anasema "hela inazagaa",na hata akiitisha harambee,anavuka malengo ya kile alichokusudia kukusanya.

Na hii inawastua wengi,sababu siku moja kabla ya kauli hiyo,kuna watu walitembelewa nyumbani kwao.Dhumuni la ujio wa ugeni ilikuwa ni "kutoa pole ya msiba".Na hakika si tu pole,baada ya pole huwa na habari za mengineyo,hayo mengineyo hubaki kuwa siri ya mfiwa na mfariji.Waunganisha matukio wanaweza kuunganisha hizi kauli na ujio wa "kutoa pole".Na wakishaunganisha,basi wanarudi nyuma katika maandishi ya kitabu cha "How The Church and Government Got The Same Bed"

Wakati wa utawala wa Kifashisti kule Italia,Mussolini aliona tishio la Kanisa Katoliki ktk kufikia malengo yake.Maana kwa wakati ule,kanisa lilikuwa na "kontroo "ya maisha ya kiroho na serikali ilikuwa na "kontroo" ya maisha ya kisiasa.

Alichokifanya Mussolin ni kujipendekeza kwa kanisa na kutoa "rushwa" ili yote atakayoyafanya kanisa katoliki lililokuwa na nguvu sana Italia libaki kimyaa.Alifanikiwa...

Kwanza aliamua kumbatiza mwanae wa kiume,ambaye hapo awali hakuwa amebatizwa.Hapa akaliteka kanisa kwa karata ya kwanza.

Pili alimua kufunga ndoa ya kikanisa,baada ya kuwa amekaa miaka 11 na ndoa ya "bomani" na mkewe Rachele.Hii ikawa karata ya pili ya kujisogeza na kujiweka karibu na kanisa ili kutimiza malengo yake ya ufashisti.

Karata nyingine;aliamuru kufungwa kwa maduka yote ya vileo(wine shops) na kufuta leseni za clabu zote za usiku ili kuendana na kauli ya kanisa ya kupunguza uovu mitaani kwa ulevi na anasa za usiku.Hapa kanisa katoliki likanasa mtegoni.

Alienda mbali mpaka akatangaza kuwa "Public Swearing" kama "Public Crime"...Yaani mwananchi ukiwa mtaani umnabishana,mtu akikwambia sema haki ya Mungu...Ukisema tu "Haki ya Mungu ntayafunga majizi yote,msema kweli ni mpenzi wa Mungu".Basi ujue wewe una kesi ya jinai ya kujibu.Hapa alitaka kulifurahisha kanisa kwa amri ile ya "Usitaje bure jina la bwana Mungu wako"(Kwa hiyo amri hiyo ingekuwa enzi hizi,kuna mtu angekuwa jela zamaniii(kidding))

Mussolini akaamuru kupigwa marufuku vidonge vya majira na kampeni zote za matumizi ya uzazi wa mpango kama ulivyo msimamo wa kanisa.Wakati huo wa 1920's kanisa lilitaka wanawake wabaki nyumbani ili kulea watoto na kukuza familia vyema.Mussolini akalipigia chapuo hili na kulitungia sheria ili kuwafurahisha wazee wa kanisa.

Akatunga sheria ambayo ilifutilia mbali talaka kwa ndoa hata za bomani.Hii ilikuwa ni njia ya kuungana na kanisa ktk ndoa ya mke mmoja na isiyo na talaka mpaka Mungu awatenganishe.Ndoana hii ikanasa vizuri kwa kanisa.Hawakupepesuka wala kutikisika.Mambo yote ya ndoa yakaondolewa serikalini na kubaki kuwa in "Full Control of the Catholic Church".Wale wapenda mteremko wa ndoa za bomani wakakosa pa kwenda.

Akatoa 109 acres ktk mji wa Roma ili yajengwe makao makuu ya Papa(Vatican) baada ya kuwa yalipokonywa wakati wa "Unification of Italy" ya miaka ya 1870's,na akaamuru kanisa lilipwe zaidi ya £130 milioni kwa wakati ule.Hii ilikuwa ni ndoano iliyoingia sawasawa kwa kanisa,na kanisa halikusema lolote juu ya "ufashisti" wa Mussolini hadharani;japo liliouona na kuuhisi kwake na kwa waumini wake.

Vatican ikawa nchi ndani ya mji,wakapewa mamlaka juu ya Post Office,jeshi dogo,polisi na "Rail station".Baada ya hapo,ugomvi ukawa ni nani anatakiwa "kukontrol" Elimu?Mussolini alihitaji elimu ili apandikize "ufashist" kwa watoto,na kanisa lilitaka elimu ili kupandikiza "dini" kwa watoto.

Mambo haya yote ambayo baadae,waumini wasio "rasharasha" waliona ni kama "rushwa" kwa kanisa ili liweze kusifia na kukaa kimya juu ya "serikali ya kifashisti" ya Mussolin yalifanikiwa.Si ajabu Papa John Paul II alikuja kuiomba jumuiya ya waumini na wasio waumini ktk jubilei ya miaka 2000 ya Ukristo kwa yale yote kanisa iliyoyakosea ktk kukuwa kwake.

Hakukuwa na Kardinali,askofu wala kasisi(padre) aliyeikemea serikali isiyo ya kidemokarasia ya Utawala wa Mussolini.Mengi yalitokea na kanisa lilikaa kimyaaa.Waumini waliteseka,waliumia na walipata machungu ya maisha...Lakini kanisa lilisema "hewalaaa",huu ni utawala mzuri tu,maana "umerudisha" heshima ya Papa katika nchi ya Italia.

Hatumaanishi kuwa sasa Tanzania tuna "ufashisti",lakini tunakubaliana kuwa kwa sasa Tanzania maisha ni magumu,pesa imepotea na uchumi umenyambulika na kutikisika.Hii inaweza kuwa ni matokeo ya kipindi cha mpito kuelekea uchumi wa viwanda,lakini haiwezi kuwa sababu ya kutokusema ukweli kuwa "HALI NI NGUMU"

Kama hali hii ni kwa sababu mianya yote ya wapiga dili imefunikwa basi na tusema,na sio kusema kinyume chake.Kuwa baba wa kiroho na kuongea kinyume cha yale waumini wako ambao ni sehemu ya wananchi wa Tanzania wanalalamika,ni kuwa upande wa pili badala ya ule wa waumini wako.

Ndio maana wale wanafunzi wa historia ya kale,wanaweza kustuka.Kwamba kauli hii inakuja siku kadhaa baada ya mtu kutembelewa nyumbani kwake,inaweza kuwatia watu woga.Kanisa libaki kuwa mali ya waumini wanyonge,liachane na "urafiki" wa mashaka kama ule wa "Mussolini" na "Vatican" enzi hizo za zama za giza za Ulaya.

Kama kanisa la wakati huo lilibaki kimya juu ya "ufashisti" wa Benitho Mussolini,hili la kwetu la Tanzania,lisibaki kimya juu ya "Ugumu wa maisha na hali mbaya ya Uchumi" kwa waumini wake.Kutoa kauli za aina hii hadharani,mbele ya mimbari na katika altare takatifu,inatupa mashaka na tutaamua kurudi na kupekua kurasa za kitabu cha "How The Church and Government Got The Same Bed"

Tukizifunua kurasa hizi;Tutahitimisha kwa kusema "Pengo ameongea lile alilotumwa kuongea na sio alilojituma kulitumikia"

Tutamkumbusha Pengo kuwa kuutumikia mwili ni ghalama zaidi ya kuitumikia roho.Ndio maana Lugha Mama ya Kanisa ya Kilatini ikasema "Nemo Liber Est Qui Corpori Servit"(No One is Free who is a slave of his body)

Tuitumikie Roho inayodumu milele,kuliko mwili unaooza na kuliwa na nyenyere.
Umeeelezea vzuri sana sana!!
 
THE ANIMAL FARM...walioshiba hawajui shida za wenzao..hawa jamaa ukifatilia mambo yao ya JESUITS,OPUS DEI unakata tamaa kabisa na dhehebu hilo hata kwa Hitler walimsaidia sana kufanya aliyoyafanya
 
Mimi mwenyewe sijaamini kama kusema hivyo alikuwa amedhamiria,, inawezekana maneno yalimtoka bahati mbaya.. ila hata kipindi fulani maaskofu walitoa waraka juu ya katiba mpya, ila yeye akaja kupingana nao.. Mungu atusaidie sana..
Aliipata fresh kutoka kwa Gwajima
 
THE ANIMAL FARM...walioshiba hawajui shida za wenzao..hawa jamaa ukifatilia mambo yao ya JESUITS,OPUS DEI unakata tamaa kabisa na dhehebu hilo hata kwa Hitler walimsaidia sana kufanya aliyoyafanya
Siyo hvyo tu.... Nawasihi tusome tena biblia kwa wale wakristo (vitabu vya Daniel, Ufunuo na Ezekiel ) kwa umakini na kufuatilia vizuri unabii na historia na ndipo utalielewa vzr kanisa katoliki duniani na siyo Tanzania pekee..ya kuwa Maneno ya Pengo aliyatoa kwa bahati mbaya au alidhamiria?!
 
  • Thanks
Reactions: SDG
View attachment 451096

Mkuu ongezea na hivi...Jaribu kuvitafuta;au nikipata wasaa huku nilipo nitakununulia ila uwe tayari tu "kurefund"....Ukisoma hivi,si tu utajielimisha,bali pia imani yako itakuwa,na hutaiegemeza kwa mtu(binadamu/Kiongozi wa dini).

Bali imani yako itaidumisha ktk Kanisa moja,katoliki la mitume...Ambalo lenyewe litaendelea kuwepo na hawa wengine watakuja na kupita.Maana tuliambiwa...Hili ndio Kanisa alilokabidhiwa Petro,na baadae akawaachia makhalifa wake,ambao ndio hao Mapapa...
View attachment 451095
Nilikuja inbox mkuu.. naomba ureply if posible
 
Back
Top Bottom