Kauli hii ya Makamu Rais wa Kenya Rutto huenda ikasababisha machafuko muda wowote huko Kenya

Kauli hii ya Makamu Rais wa Kenya Rutto huenda ikasababisha machafuko muda wowote huko Kenya

Exactly Mkuu. Kama inapingana na Kenyatta alisema andamaneni kwa amani
 
Kama kenya kutakuwa na vita basi Raila na NASA wameshiriki Kwa Kiasi kikubwa kuanzisha
Tuliwaambia zamani miaka kumi (2007-2008 PEV) kwamba Raila ndiye alikuwa chanzo cha machafuko Kenya hamkuamini.Yule jamaa ni mchochezi na mtu mwenye ubinafsi sana.
 
Ni kauli ambayo Makamu Rais wa Kenya Mheshimiwa William Rutto aliyoitoa muda si mrefu ambayo imeonekana kuwakera Wakenya wengi huku wengine sasa wakisikika kwamba wako tayari kwa Vita muda wowote kwani hiyo kauli ni Kiashirio tosha kwamba akina Kenyatta na Rutto wanataka Vita / Machafuko nchini Kenya.

Kauli yenyewe ni hii hapa nainukuu...." Tuliwaonya hawakutusikia sasa Chuma chenu Kiko motoni na muda si mrefu Kitaungua chote ili Kenya ibaki kuwa salama kwani tumechoka na tumewachoka " mwisho wa kuinukuu.

Kwa undani zaidi wa hiyo Kauli ingia katika Mtandao wa Standard Digital upate uhondo kamili. Labda nitoe tu Rai kwa Wakenya kwamba hapa East Africa hatutaki Vita au Machafuko hivyo wamalizane tu kwa amani na kwa kupiga Kura na siyo kwa mapigano.

Nawasilisha.
Afadhari ya maneno hayo na watu wakaelewa kuwa vita inakuja kuliko na wakajipanga kuliko vita vya kimya kimya vinavyoendelea katika nchi ya kusadikika na tukiendelea kushuhudia viroba vya maiti vikiopolewa baharini,hii ndio vita mbaya zaidi.
 
Back
Top Bottom