Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Pamoja na siku za hivi karibuni kutoa boko sana kwenye hotuba zake lakini this time inaonekana kama Rais Samia ameanza kurudi kwenye mstari.
Kuna kauli ameitoa akiwa akiwa huko na Namtumbo, kauli ambayo bila shaka itachagiza wanawake wengi hasa wa vijijini kupiga kura kwenye uchaguzi ujao.
Wakati anazindua shule ya wasichana huko Namtumbo mkoani Ruvuma, Rais Samia amezungumzia kuhusu nishati safi ambapo amedokeza kuwa ana mpango wa kuwasaidia wanawake wengi kuacha kutumia kuni ili waanze kutumia nishati safi kama vile gesi n.k
Soma pia: Rais Samia Ameibeba Ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia Kimataifa
Kwa wale ambao wameshaishi vijijini bila shaka watakuwa wanafahamu jinsi ambavyo matumizi ya kuni yanaathiri afya za wanawake na kauli hii ya Rais Samia ni kama imekuja kuwakomboa wanawake hao.
Rais Samia amesema:
Kwenye hili, Rais ameupiga mwingi kwani wanawake wengi bila shaka watajitokeza kupiga kura ili waweze kujitoa kwenye matumizi ya kuni.
Nawasilisha

Wanawake wa Afrika wanapata maradhi kwa sababu wanapikia kuni. Wanakufa na maradhi ya kupumua, wanapofua macho na hiyo ni kwa sababu kuni zinatoa gesi mbalimbali ambazo zinawapa madhara mama zetu, bibi zetu waliumia sana kwenye hilo. Sasa wakati umefika tubadilishe tutumie nishati safi za kupikia.
Kwa sababu mradi huu lengo lake ni kuwa ifikapo mwaka 2030, asilimia 80 ya watanzania wawe wanatumia nishati safi.