Kauli hii ya wanawake "Nimempa kila kitu still kaniacha"

Kumbe ni ngono tu,mi nikajua wanawapa tundu zote mbili...maana hiyo kilakitu imetrend sana
 
Mkuu anzisha thread bana,tuambie ilikuaje
Pole sana lakini
 
Pole sana mkuu umeongea kwa msisitizo wa kubold kabisa.
 
Ndugu yangu em paki Gari pembeni utupe huu Mkasa
 
Ndugu yangu em paki Gari pembeni utupe huu Mkasa
2010 hiyo nilikuwa na mtoto wa kichaga mmoja hivi matata sana,, na mi nilikuwa mshamba kidogo wa mapenzi nikazama miguu yote,, nikawa na mpango wa kabisa wa kuoa..

Basi akapata nafasi ya Degree ya Ualimu hapo UDOM,, shida alikuwa na mama tu ambaye hakuwa vizuri kiuwezo ( dingiake alishavuta kitambo )kwahiyo kidume nikaamua kujibebesha majukumu ya ubaba nikagharamikia Ada iliyobaki maana alipata 30% ya mkopo na shopping za hapa na pale na hiyo Laptop.

Miezi miwili ya mwanzo mawasiliano yalikuwa poa yaani weekend nyingi nipo UDOM EDUCATION BLOCK "N" ROOM No. 50+ kumtembelea mke mtarajiwa.
Baada ya miezi kama minne hivi simu zikaanza kutokupokelewa na mesej hazijibiwi... Nikaona siyo kesi, nikaenda mwenyewe ghafla bila kumtaarifu, kufika tu chumbani Block N nikagonga hodi akafungua mwenzake mara namwona kipenzi kabambiwa na sharobaro kwenye kitanda chake na mkao wa kihasara kabisa, yaani haihitaji kuuliza ukaribu uliopo,, niliduwaa kama sekunde flani pale mlangoni , naye hakusema neno akabaki na mshangao na jamaa yake akawa anashangaa,,,, nikafunga mlango nikatoka zangu nje nikawa naondoka nashuka ngazi,,, mara akanifuata kwa nyuma na maelezo nisifikirie vibaya nilichokiona sijui na mengine hata sikumbuki...

Nikapanda ki-hiace mpaka Jamatin ndo nikaenda stendi kubwa pale pa zamani,,, nimekaa zangu nawaza jinsi nilivyokuwa mjinga kwa miaka 4 nahudumia chuma ulete .. nilikaa kuanzia saa 10 jioni mpaka saa 4 usiku hivi nawaza na kuwazua.... baadaye nikapanda basi linalotoka Tarime nikaja zangu Dar na ndo mpaka leo hatujawahi kuwasiliana..

Kuanzia hapo nikawa mtu mpya...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…