Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 1,831
- 5,489
Jamaa aliyepata umaarufu mitandao kwa uuzaji wa Kitimoto alimaarufu kama nguruwe atimbiwa na Bodi ya Nyama iliyochini ya Serikali. Bodi hiyo imefika katika eneo la Bwana huyo ambaye pia ni maarufu kwa jina la Mr. Manguruwe na kukagua maneno ya banda hilo la nguruwe. Alianza kupata umaarufu baada ya kuahidi kumpatia Mchezaji wa Simba Clatous Chama endapo atafunga Goli. Mfugaji huyo alisikiaka na kujizolea umaarufu kwa kushawishi watu kula nyama ya kitimoto na kusema kitimoto inasaidia kuongeza maumbo ya wanawake, na pia akisema kitimoto wake ni wa kipekee na wamenona, jambo lililopelekea serikali kupitia bodi ya nyama kuamua kutia kambi katika eneo lake.
Ukisikiliza kwa umakini utagundua wawikilishi hapo wapo kwa ajili ya kuiua biashara ya mfugaji huyo, kauli za kufukuza wateja badala ya kumuhamasisha na kumtia nguvu.
View: https://www.instagram.com/reel/C7HQZEEieqh/?igsh=MWI2dHpjMnFybHF4OA==