Uchaguzi 2020 Kauli Mbiu ya CHADEMA: Uhuru, Haki na Maendeleo ya watu

Umeona mkuu, hawa jamaa chenga kweli, eti wanajivunia kuifanya nchi dampo la bidhaa kutoka nje, Magufuli anahamasisha viwanda wao wanakuja na mbadala wa kufuta kodi 15 kwa wafanyabiashara na kufanya bidhaa kutoka nje zimwagike nchini, hawajui moja ya sababu ya colonialism hata watoto wa Sekondari wanasoma ilikuwa ni kutafuta sehemu ya kumwaga bidhaa zao za viwandani, hatutarudi kuwa koloni tena.

Kwani sasa hazingii nenda k/koo madukani ukaone tumia elimu na maarifa
 
Uhuru hadi kwenye ushoga. Mtaipenda kama siyo kukoma.
 
Wasalaam wakuu,
Poleni sana na shughuli mbalimbali za kujenga taifa.

Sote katika jukwaa la siasa tumekwisha shuhudia la mgambo likilia kwa vyama mbalimbali kuanza kampeni za uchaguzi wa tarehe 28, oktoba 2020.

Tayari vyama vimekwisha anza kunadi sera zao kupitia wagombea wao. Binafsi nimefurahishwa sana na ilani ya chama cha demokrasia na maendeleo, CHADEMA. Kufurahishwa kwangu huko kumetoka na sera zao ambazo kiukweli zinagusa uchumi wa taifa letu(MACROECONOMICS) na pamoja na uchumi wetu sisi wananchi mmoja mmoja (MICROECONOMICS).

Sera za CHADEMA zenye fungamanisho la sekta ya umma na sekta binafsi (PPP or public-private partnership) ni nguzo katika kukuza uchumi wa nchi na uchumi wa watu wake.

Katika sera hizi mgombea wa CHADEMA nafasi ya Urais Mh. Tundu Antipas Lissu ameanza kuelezea vyema utekelezaji wa sera hizi atakazozisimamia katika kipindi chake cha utawala wa miaka mitano( 2020-2025).

Sera hizi zimekwisha anza kupokelewa na watu wengi maana zinagusa kila kundi ikiwa ni pamoja na Wafanyakazi, Wakulima, Wajasiriamali, Wawekezaji, Wasomi na Wanafunzi wa elimu kuanzia msingi mpaka vyuo vikuu.

Summary ya Sera za CHADEMA katika ilani yake ya 2020:

1.Katiba Mpya (ikiyasimamia maoni ya kamati ya Warioba)

2. Uhuru wa vyombo vya habari.

3. FAO LA KUJITOA LINARUDI
-ukiwa na utayari wa kusitisha mkataba wa kazi, utapokea mafao yako kulingana na mfuko wako mafao.

4. Maduka yasiyotozwa Kodi jeshini yanarudi.

5. Riba za mikopo ya elimu ya juu itashuka kutoka 13% mpaka 3%.

6. Sheria kandamizi zote zenye upendeleo kwa makundi fulani zitafutwa.

7. Maendeleo yatalenga watu na si vitu, kwamba ili nchi ipate maendeleo lazima kwanza watu wake waendelezwe kielimu(maarifa na ujuzi), kiafya na malazi(makazi Bora).

8. Kodi ya ongezeko la thamani VAT itakua 10% kutoka 18% ya Sasa hivi, ili kuchochea na kurudisha matumaini ya watu kurudi katika biashara na kuongeza uzalishaji mali na hivyo kuinua pato la Taifa.

9. Kodi ya ardhi itapunguzwa ili kuifufua sekta ya makazi ambayo katika kipindi hiki cha miaka mitano imefifia.

10. Kupandisha madaraja na mishahara ya wafanyakazi; swala ambalo lipo kisheria na litafanywa na serikali ya CHADEMA chini ya Rais wake Mh. Tundu Antipas Lissu.

11. Mazingira Bora ya uwekezaji. CHADEMA imepanga kuboresha mazingira mazuri ya uwekezaji ikitumia mbinu ya ubia wa sekta ya umma na binafsi katika kuwavutia wawekezaji kupitia punguzo la kodi na uendelezwaji, ufufuaji na uanzishwaji wa maeneo maalum ya kimkakati ya kiuchumi yaani SEZ(Special Economic Zones).

12. Matibabu kwanza malipo baadae; Kupitia bima ya Afya kwa wananchi wote serikali ya CHADEMA imejiandaa kutoa bima kwa wananchi wote ili kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma ya Afya bora katika muda wote. Hii itapunguza vifo ambavyo mara kadhaa vimesababishwa na wagonjwa kukosa fedha za matibabu kwa wakati.

13. Kodi ya wafanyakazi kwenye mshahara (PAYE) haitazidi 8%. Serikali ya CHADEMA chini ya Mh. Tundu Antipas Lissu imepanga kutoza kuchukua kodi ya PAYE isiyozidi 8% ili kupunguza kodi kubwa ambayo ni mzigo kwa Wafanyakazi.

14. Masharti ya mikopo kwa Vijana itakua nafuu. Wanafunzi wa elimu ya juu hawata daiwa madeni yao waliyokopeshwa na HESLB mpaka pale watakapoajiriwa either katika sekta ya umma ama binafsi.

15. Upatikanaji wa Maji Safi na salama kwa gharama nafuu. Serikali ya CHADEMA ikishirikiana na sekta binafsi imejipanga kusambaza na kutengeneza miundombinu ya maji Safi na salama kwa ustawi wa Watanzania.

16. kuboresha miundombinu vijijini. Vijijini ikiwa ndiyo sehemu inayokaliwa na watu wengi ambao ni wazalishaji wa Chakula na malighafi kwa ajili ya viwanda, serikali ya CHADEMA chini ya Mh. Tundu Antipas Lissu imepanga kuimarisha miundombinu vijijini ili kuunganishwa maeneo ya kimkakati ya uzalishaji malighafi shambani na bidhaa viwandani.

Nawasilisha haya machache.

#Mpiga-kura_huru
#Uchaguzi2020
#TUKAPIGE_KURA
#TANZANIA-AFRICA
#VISION2025
#AGENDA2063

View attachment 1552566View attachment 1552568View attachment 1552569View attachment 1552570View attachment 1552571View attachment 1552572
Sera nzuri sana inafurahisha hongereni sana CDM tupo nanyi.
 
Mleta mada nikupongeze walau kwa kuleta hiyo ilani nashukuru hiki ndicho wananchi wataka kukisikia hongera kuitoa sababu mikutano ya Chadema ilikuwa imejaa porojo tu Lisu anapiga porojo hewa za kutunga kichwani mwanzo mwisho

Nikushukuru Tena ni matumaini yangu kuwa hizo mtazinadi kwenye majukwaa hazitaushia Jamii forums ili.muondokane na aibu ya porojo majukwaa
Nina reservation nyingi kwenye hiyo ilani ila kwa Sasa niwapongeze walau mna kakitu ka kuongelea hata Kama Ni la ilani hewa hewa

Nitaichambua baadaye ngoja ninywe chai
 
Lisu na Mbowe huo Uhuru , haki na maendeleo wameshindwa kuleta ndani ya CHADEMA yao ndio wataweza kuwaletea watanzania wote?

Na msijifanye mmesahau kumbukeni kuwa mna laana ya dk Slaa
 
Mapungufu kwenye sera ya Chadema

1.Masuala ya madini haijagusa kabisa!!! Naona ike aibu ya MIGA Chadema waneona waichomoe kimya kimya isiwe kesi

2.Uhuru wa habari Chadema haupo sababu wanataka vyombo vya habari visiwe na Uhuru wa kutangaza kile vinavyotaka Bali watangaze kile Chadema eanachotaka.Mfano TBC walifukuzwa sababu walikataa kutangaza kile Chadema wanachotaka.Kuwa lazima watangaze like Chadema wanachotaka!!! Uhuru wa habari Ni pamoja na kutoa Uhuru kwa chombo Cha habari kutangaza kinachotaka.Huo Uhuru sio one way traffic Ni two way traffic . Chadema kwa hili wameshindwa kwa kuinyima Uhuru TBC kutangaza wanachokitaka Kama sehemu yao ya uhuru wa habari .Kwa Chadema Uhuru wa habari maana yake Ni wao ndio wenye haki ya kusema kitangazwe kipi na chombo Cha habari.Chombo Cha habari hakina huo Uhuru wa kujiamulia kitangaze Nini

3.Kuhusu wafanyakazi wa umma kupandishwa mishahara na madaraja Chadema wamechemka wanasema watapandisha na kulipa malimbikizo hii sera imepitwa na Wakati wafanyakazi wa umma wamekuwa wakipandishwa mishahara na madaraja kimya kimya kuepuka mfumuko wa bei mitaani .Mishahara na vyeo kupanda Ni Siri Kati ya mwajiri na mwajiriwa .Wamekuwa wakipandishwa na kulipwa malimbikizo kimya kimya maofisini hivyo Chadema mkinadi hii sera wafanyakazi wa umma wataangua vicheko kuwa mnanadi vitu hewa!!!

Sasa hivi nyongeza haxitangazwi zilikuwa zikiyangazwa tu kesho Bei za vitu juu Ni strategy ya awamu ya tatu kudhibiti mfumuko wa Bei naona Chadema mko gizani au Kuna mtu kawapa hii kuwahujumu muangukie pua kwenye kampeni!!!
 
Ni bora, tuko huru na tuko na maamuzi na mambo yetu wenyewe..na bado vinaendela kujengwa.
Hatuja wahi kuwa huru chini ya CCM, kuchaguliwa viongozi wa kutuongoza, wapinzani kuteswa, kuwekwa ndani na kufungwa jela. Rais anafanya maamuzi kama Sultan.
 
Mapungufu kwenye sera ya Chadema

1.Masuala ya madini haijagusa kabisa!!! Naona ike aibu ya MIGA Chadema waneona waichomoe kimya kimya isiwe kesi

2.Uhuru wa habari Chadema haupo sababu wanataka vyombo vya habari visiwe na Uhuru wa kutangaza kile vinavyotaka Bali watangaze kile Chadema eanachotaka.Mfano TBC walifukuzwa sababu walikataa kutangaza kile Chadema wanachotaka.Kuwa lazima watangaze like Chadema wanachotaka!!! Uhuru wa habari Ni pamoja na kutoa Uhuru kwa chombo Cha habari kutangaza kinachotaka.Huo Uhuru sio one way traffic Ni two way traffic . Chadema kwa hili wameshindwa kwa kuinyima Uhuru TBC kutangaza wanachokitaka Kama sehemu yao ya uhuru wa habari .Kwa Chadema Uhuru wa habari maana yake Ni wao ndio wenye haki ya kusema kitangazwe kipi na chombo Cha habari.Chombo Cha habari hakina huo Uhuru wa kujiamulia kitangaze Nini

3.Kuhusu wafanyakazi wa umma kupandishwa mishahara na madaraja Chadema wamechemka wanasema watapandisha na kulipa malimbikizo hii sera imepitwa na Wakati wafanyakazi wa umma wamekuwa wakipandishwa mishahara na madaraja kimya kimya kuepuka mfumuko wa bei mitaani .Mishahara na vyeo kupanda Ni Siri Kati ya mwajiri na mwajiriwa .Wamekuwa wakipandishwa na kulipwa malimbikizo kimya kimya maofisini hivyo Chadema mkinadi hii sera wafanyakazi wa umma wataangua vicheko kuwa mnanadi vitu hewa!!!

Sasa hivi nyongeza haxitangazwi zilikuwa zikiyangazwa tu kesho Bei za vitu juu Ni strategy ya awamu ya tatu kudhibiti mfumuko wa Bei naona Chadema mko gizani au Kuna mtu kawapa hii kuwahujumu muangukie pua kwenye kampeni!!!
Kama vyombo vya habari vingekua huru Magifuli asingehangaika kuangalia hotuba za Lissu kwenye groups za whatsup.

Kama wafanyakazi wangepandishwa mishahara kimya kimya wasingekua wanalalamika.

haya yote ni kama vile viwanda hewa 600 mlivyojenga.
 
Usawa huu kweli alofanya Magufuli kuna Mtanzania wa kudanywa!! Yan wapinzani mkifkisha kura milioni 3.5 mfanye na sherehe kabisa maana vitu vilivyofanywa na Magufuli kwa Mtanzania yoyote mwenye akili timamu awez kupoteza kula yake kuwapa wapinzani tena waliotetea mabeberu hili waendelee kubeba madini yetu bule.
 
Umeona mkuu, hawa jamaa chenga kweli, eti wanajivunia kuifanya nchi dampo la bidhaa kutoka nje, Magufuli anahamasisha viwanda wao wanakuja na mbadala wa kufuta kodi 15 kwa wafanyabiashara na kufanya bidhaa kutoka nje zimwagike nchini, hawajui moja ya sababu ya colonialism hata watoto wa Sekondari wanasoma ilikuwa ni kutafuta sehemu ya kumwaga bidhaa zao za viwandani, hatutarudi kuwa koloni tena.
Viwanda vinahamasishwa au vinajengwa?.Hebu nitajie basi ata hivyo vinavyohamasishwa tuvijue.
 
Kama vyombo vya habari vingekua huru Magifuli asingehangaika kuangalia hotuba za Lissu kwenye groups za whatsup.
Na nyie Chadema Kama mnapenda Uhuru wa habari kwa Nini mlitaka TBC watangaze mnachotaka nyie? Si mungeacha watangaze watakacho sababu ndio Uhuru wenyewe wa habari kwa Nini mliwadhibiti na kueafukuza wasitumie Uhuru wao was kutangaza watakacho?
 
.

Kama wafanyakazi wangepandishwa mishahara kimya kimya wasingekua wanalalamika.
Wanalalamika wapi? Tatizo nililoliona kwenya sera za Chadema mengi wamechukua humu jamii Forums !!! Mitandao sio reliable source hasa jamii Forums.Mengi wamebeba humuna kuyageuza sera ukienda kwenye uhalisia sio kweli likiwemo Hilo la yanayoitwa malalamiko ya wafanyakazi!!

Chadema wameshindwa kufanya homework yao kabla ya kutengeneza hiyo sera want rely jamii forums tu
 
Na nyie Chadema Kama mnapenda Uhuru wa habari kwa Nini mlitaka TBC watangaze mnachotaka nyie? Si mungeacha watangaze watakacho sababu ndio Uhuru wenyewe wa habari kwa Nini mliwadhibiti na kueafukuza wasitumie Uhuru wao was kutangaza watakacho?
Kuna faida gani ya TBC kuwepo pale wakati Lema au Lissu akiongea wanazima sauti?
 
Wasalaam wakuu,

Poleni sana na shughuli mbalimbali za kujenga taifa.

Sote katika jukwaa la siasa tumekwisha shuhudia la mgambo likilia kwa vyama mbalimbali kuanza kampeni za uchaguzi wa tarehe 28, oktoba 2020.

Tayari vyama vimekwisha anza kunadi sera zao kupitia wagombea wao. Binafsi nimefurahishwa sana na ilani ya chama cha demokrasia na maendeleo, CHADEMA. Kufurahishwa kwangu huko kumetoka na sera zao ambazo kiukweli zinagusa uchumi wa taifa letu(MACROECONOMICS) na pamoja na uchumi wetu sisi wananchi mmoja mmoja (MICROECONOMICS).

Sera za CHADEMA zenye fungamanisho la sekta ya umma na sekta binafsi (PPP or public-private partnership) ni nguzo katika kukuza uchumi wa nchi na uchumi wa watu wake.

Katika sera hizi mgombea wa CHADEMA nafasi ya Urais Mhe. Tundu Antipas Lissu ameanza kuelezea vyema utekelezaji wa sera hizi atakazozisimamia katika kipindi chake cha utawala wa miaka mitano( 2020-2025).

Sera hizi zimekwisha anza kupokelewa na watu wengi maana zinagusa kila kundi ikiwa ni pamoja na Wafanyakazi, Wakulima, Wajasiriamali, Wawekezaji, Wasomi na Wanafunzi wa elimu kuanzia msingi mpaka vyuo vikuu.

Summary ya Sera za CHADEMA katika ilani yake ya 2020:

1. Katiba Mpya (ikiyasimamia maoni ya kamati ya Warioba)

2. Uhuru wa vyombo vya habari.

3. FAO LA KUJITOA LINARUDI
-ukiwa na utayari wa kusitisha mkataba wa kazi, utapokea mafao yako kulingana na mfuko wako mafao.

4. Maduka yasiyotozwa Kodi jeshini yanarudi.

5. Riba za mikopo ya elimu ya juu itashuka kutoka 13% mpaka 3%.

6. Sheria kandamizi zote zenye upendeleo kwa makundi fulani zitafutwa.

7. Maendeleo yatalenga watu na si vitu, kwamba ili nchi ipate maendeleo lazima kwanza watu wake waendelezwe kielimu(maarifa na ujuzi), kiafya na malazi(makazi Bora).

8. Kodi ya ongezeko la thamani VAT itakua 10% kutoka 18% ya Sasa hivi, ili kuchochea na kurudisha matumaini ya watu kurudi katika biashara na kuongeza uzalishaji mali na hivyo kuinua pato la Taifa.

9. Kodi ya ardhi itapunguzwa ili kuifufua sekta ya makazi ambayo katika kipindi hiki cha miaka mitano imefifia.

10. Kupandisha madaraja na mishahara ya wafanyakazi; swala ambalo lipo kisheria na litafanywa na serikali ya CHADEMA chini ya Rais wake Mh. Tundu Antipas Lissu.

11. Mazingira Bora ya uwekezaji. CHADEMA imepanga kuboresha mazingira mazuri ya uwekezaji ikitumia mbinu ya ubia wa sekta ya umma na binafsi katika kuwavutia wawekezaji kupitia punguzo la kodi na uendelezwaji, ufufuaji na uanzishwaji wa maeneo maalum ya kimkakati ya kiuchumi yaani SEZ(Special Economic Zones).

12. Matibabu kwanza malipo baadae; Kupitia bima ya Afya kwa wananchi wote serikali ya CHADEMA imejiandaa kutoa bima kwa wananchi wote ili kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma ya Afya bora katika muda wote. Hii itapunguza vifo ambavyo mara kadhaa vimesababishwa na wagonjwa kukosa fedha za matibabu kwa wakati.

13. Kodi ya wafanyakazi kwenye mshahara (PAYE) haitazidi 8%. Serikali ya CHADEMA chini ya Mh. Tundu Antipas Lissu imepanga kutoza kuchukua kodi ya PAYE isiyozidi 8% ili kupunguza kodi kubwa ambayo ni mzigo kwa Wafanyakazi.

14. Masharti ya mikopo kwa Vijana itakua nafuu. Wanafunzi wa elimu ya juu hawata daiwa madeni yao waliyokopeshwa na HESLB mpaka pale watakapoajiriwa either katika sekta ya umma ama binafsi.

15. Upatikanaji wa Maji Safi na salama kwa gharama nafuu. Serikali ya CHADEMA ikishirikiana na sekta binafsi imejipanga kusambaza na kutengeneza miundombinu ya maji Safi na salama kwa ustawi wa Watanzania.

16. kuboresha miundombinu vijijini. Vijijini ikiwa ndiyo sehemu inayokaliwa na watu wengi ambao ni wazalishaji wa Chakula na malighafi kwa ajili ya viwanda, serikali ya CHADEMA chini ya Mh. Tundu Antipas Lissu imepanga kuimarisha miundombinu vijijini ili kuunganishwa maeneo ya kimkakati ya uzalishaji malighafi shambani na bidhaa viwandani.

Nawasilisha haya machache.

#Mpiga-kura_huru
#Uchaguzi2020
#TUKAPIGE_KURA
#TANZANIA-AFRICA
#VISION2025
#AGENDA2063

View attachment 1552566View attachment 1552568View attachment 1552569View attachment 1552570View attachment 1552571View attachment 1552572

Sera nzuri sana.
 
Sio watabeza, ni takataka, alisema atafuta kodi, kwamba Leo kuna kodi 15 kwa wafanyabiashara na hazitaji, kwamba akifuta kodi bidhaa kutoka nje zitamwagika nchini, nani alimwambia tunahitaji kurudi kwenye ukoloni wa kuifanya nchi yetu dampo la bidhaa za mabeberu? UPUUZI.
Hoja haipigwi rungu mkuu. Jikite kwenye hoja.
 
Back
Top Bottom