Kauli Mbiu ya Mei Mosi mwaka huu 2025 ni Fumbo kwa Rais

Kauli Mbiu ya Mei Mosi mwaka huu 2025 ni Fumbo kwa Rais

Gai da seboga

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2019
Posts
532
Reaction score
1,037
Wasalam Mabibi Na Mababu!

Bila kupoteza muda Kauli mbiu ya Mei Mosi-2025 ni;

''Uchaguzi mkuu 2025, utuletee viongozi wanaojali haki na maslahi ya wafanyakazi, sote tushiriki.''

Nadhani Mheshimiwa Raisi anahitaji mtaalamu wa fasihi na lugha aweze kumfumbulia hili Fumbo.

Nachoona wafanyakazi mwaka huu wameamua kumtumia ujumbe mzito sana baada ya kuona kuwa hajali maslahi yao kwa kuwaongezea Mishahara minono, lakini pia Dissapointment waliyopata kwenye Sherehe za mwaka jana kukimbiwa na Mkuu wa Nchi, lakini pia Kukwazika na Kauli ya kisiasa iliyotolewa na Makamu wa Nchi kuwa Mwenye nchi atasema neno juu ya nyongeza ya mshahara kwa watumishi Lakini Hoolaa mpaka mwaka mwingine umefika.

Kwa ufupi kauli mbiu hiyo ipo kifumbo zaidi yaani kama aliopo madarakani hajali sasa uchaguzi utuletee anaejali. 'Sote tushiriki' maana yake tushiriki sote kumuondoa huyu asiejali watumishi, Mana angekuwa aliyekuwepo anajali basi tusingesubiri uchaguzi tungeridhika na huyu huyu.

Nadhani Mheshimiwa ajue ukweli tu kuwa watumishi washachoka sidhani kama wanataka kusikia tena maneno ya kisiasa, cha kufanya ni kuwaongezea Mishahara watumishi ili keki ya Taifa Iwafaidishe wengi.

Nyongeza ya mishahara imekuwa donda sugu sana mpaka sasa wafanyakazi wanaamua kutumia mafumbo ili wafikishe ujumbe Hali ni Mbaya sana, Naamini Mhe ni msikivu na mwenye huruma Hakika tarehe 1/5/2025 watumishi watasikia kile kitakachowakonga nyoyo zao... Weka Nyongeza Mama Tukupe Mitano Yako
 
Kikomotoo mtihani mkuu hasa 1/540 na 1/580
 
Wafanyakazi gani hao wenye kumfumba Rais? Hawa Hawa ambao Milton yao inaichukia CCM lakini physically wanalazimika kujionyesha Kama wanaipenda kinafiki nafiki?
 
No Reform, No Election. Hii ndio kauli mbiu sasa.
 
Back
Top Bottom