Sakasaka Mao
JF-Expert Member
- Sep 29, 2016
- 16,028
- 23,380
Na nadhani aliwekwa katika nafasi ile kufubaza maovu ya iliyemteua.Nakubaliana na wewe mkuu.
Tafsiri yako ni sahihi hujakosea ila tujiulize madongo au mafumbo na mapisho kipindi hiki yanaliponya taifa? Madongo yanapunguza makali au yanaongeza chumvi kwenye kidonda?
Ndio maana nikasema tofauti yao na bosi wake ni ndogo sana wakiwa chini ya mwamvuli mmoja.
Ukatoliki pamoja na uislamu havipaswi kuwa gumzo kipindi hiki sababu watanzania hasa watanganyika wameumizwa bila kujalisha dini zao.
Tukifanikiwa kuwapuuza hao majamaa katika issue ya udini watarudi nyuma na kujitafakari upya.
Nchimbi Emmanuel muda unavyozidi kwenda atapoteza control na hao wa upande wa pili watakuwa wamefanikiwa kumvuta acheze ngoma na midundo yao bila kupenda.
Atumie udini asitumie, sidhani kama kuna mtu mwenye akili timamu anayeweza kurubunika na hizi hadaa zao!
Kama unavyosema mkuu, kuliponya taifa kwa sasa kunahitaji busara isiyohojika na si usanii wa kugawa watu wanaoufanya sasa.