LGE2024 Kauli ya Chadema ya " Watake Wasitake Tutashiriki na Kushinda" imeishia wapi? Naona wamekuwa Wapole mno kuliko enzi za Shujaa Magufuli!

LGE2024 Kauli ya Chadema ya " Watake Wasitake Tutashiriki na Kushinda" imeishia wapi? Naona wamekuwa Wapole mno kuliko enzi za Shujaa Magufuli!

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Kwa hi
Wacha visingizio..Kwenye kila sehemu walioshinda CCM walijitokeza maelfu ya watu wakishangilia ushindi walioupata.Kelele za wapinzani zilisikika sehemu chache sana wengi wao wakilalamika bila ushahidi.
Mfano kuna mtaa USA river unaitwa Mji mwema CCM wamepata kura takriban 5000 Chadema kura 120.Bado unalalama na kutafuta visingizio?
Mawakala wamejitokeza na kusema uchaguzi haukuwa na figisu. Badala ya kutafuta chanzo cha kushindwa vibaya mnaleta visingizio.
Huwezi kushinda uchaguzi bila grassroots votes.Kufanya kosa na kulirudia mara kwa mara na kutegemea matokeo tofauti ni ukichaa.
Unajifanya kusahau kuwa mlitaka kuwaengua takriban wabombea wote kutoka upinzani. Ni baada ya kuona aibu ndio mkarudisha baadhi yao. Nia ya kushinda viti vyote kwa hila mlionyesha tokea mwanzo. Na kwenye hilo mmefanikiwa.

Sasa ni wajibu wenu kuboresha maisha ya wananchi wenu kutoka pale zaidi ya miaka 60 ya utawala wenu umewafikisha. Hamna tena kisingizio kuwa wapinzani wanawazuia. Hizo nafasi mlizotangazwa kushinda zina majukumu yake. Fanyeni hima mkawatumikie wananchi wa Tanzania bara. Miaka mitano sio mingi.

Amandla...
 
Back
Top Bottom