Kauli ya Dr. Bujugo na Umalaya wa Kinondoni Watoto Wetu Wapo Salama Green Acre?

MPUNGA

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2010
Posts
838
Reaction score
561
Huyu Mheshimiwa amenukuliwa na vyombo vya habari kuwa biashara ile kongwe kuliko biashara zingine ya Umalaya ihalalishwe ili kuongezea mapato halmashauri ya wilaya ya Kinondoni.

Ni ukweli mchungu kuwa hii biashara imeshamiri kwenye wilaya ya Kinondoni , ila wasiwasi wangu ni ile kofia nyingine anayovaa kama mmiliki na mwendashaji wa Shule za Green Acre, kwa kauli kama hizi za kushododia biashara ya Umalaya tena wazi wazi na kweupe , watoto wetu kwenye hizo Shule zake wapo kweli kwenye mikono salama?

Kweli hapa tunaweza tukasema ya Kaisari mpe Kaisari?
 
jamani wasomi wetu hebu kuweni makini na kauli zenu mbona mnawaza vitu vyenye majibu rahisrahis tu. hivi kweli dokita umekaa ukaona njia ya kutibu ongezeko la pato ni umalaya? kweli ?hivi hebu vaa uhusika mwanao anakuaga anakwenda kazini kwenye umalaya au anakwambia baba niungishe leo biashara mbaya! acha u.ji.nga umesoma lakin elimu bado haijakukomboa nawasiwasi kama unaweza kuwa na mchango wa maana sana kwa jamii kwa hicho kidokta chako.
 
hizo shule zake zenyewe hazina maadili kabisa, ameruhusu wasichana kuvaa sketi fupi kupita kiasi mpaka inahamasisha ngono hasa wakikaa mapaja yanaonekana barabara,sijui wavulana pale wanasomaje, wasichana wanaruhusiwa kutengeneza nywele kama chuo wanafanya kila aina ya kujiremba, matokeo ya shule four na zero
 
Hivi huyu bwana ni msomi wa kiwango cha 'Dr' au ni zile za kununua kama mwenzao!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…