Naomba kujua kuhusu kauli hii. Mimi ninavyojua kwa uelewa mdogi nilionao wa mambo ya mahakama. Ni kwamba unaweza kufungua kesi ya jinai ila huna uwezo wa kuifuta au kumsamehe kwani hata kama umefungua kesi bado utaendelea kuhesabiwa ni shahidi. Kwa mfano ukivamiwa na mtu ukaenda kutoa taarifa. Kimsingi ni kesi ya jinai japo kuwa imasimamiwa na serikali lakini wewe uliefungua utahesabiwa kuwa ni shahidi. Kwa maana nyingine hakuna mantiki ya Slaa kukwepa kwenda kufungua kesi. Ni propaganda za kisiasa anazojua kabisa hatafanikiwa mahakamani.