Kauli ya Dullah Mbabe kupigana akiwa mgonjwa kisa kupata mkate wa familia, bodi ya ngumi mjitathmini

Kauli ya Dullah Mbabe kupigana akiwa mgonjwa kisa kupata mkate wa familia, bodi ya ngumi mjitathmini

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
9,091
Reaction score
21,087
Dullah Mbabe akasema alipiga ili watoto wapate ridhiki ya kula na shule japo ni mgonjwa na ana majeraha makubwa, hii ni kauli ya kishujaa Kwa mwanaume inauma kuona watoto wanakosa chakula na masomo ukiwa hai, laZima utafanya shughuli yoyote ya hatari watoto wapate ridhiki.

Dullah Mbabe ni kati ya mabondia maarufu Tanzania, Kwa umaarufu wake tulitarajia atakuwa na kipato cha kulisha familia na mambo yakaenda bila kihatarisha afya yake zaidi

Kupigana akiwa na majeraha ni kuzidi kujiuma na kuuwa kipaji chake ambacho ni faida Kwa Watanzania

Dullah Mbabe anatufikirisha wadau wa ngumi kuwa labda hawa vijana Huwa wanalipwa kiasi kidogo Kwa mchezo wa hatari kama boxing 🥊, huku promotors wakifaidi jasho la hawa vijana wa Kimasikini

Sasa kama Dullah Mbabe ambaye ni professional boxer anapigana akiwa na majeraha ili watoto wale itakuwaje Kwa mabondia wengine wadogo

Hii ni hujuma hata Kwa watazamaji ambao wao wanalipia kiingilio wakijua ni mchezo kumbe boxers wameenda kujitoa mhanga na wapo tayari kupigwa kikubwa wavumilie na kupata pesa ya chakula, hii sio sawa

Juzi tulitoka kumpoteza kijana aliyepigana Kwa malipo ya elf 60 na kuishia kupigwa vibaya labda sababu ya njaa na lishe mbovu yule kijana akapoteza maisha

Bodi ya ngumu tazama maslahi ya mabondia wenu, wawe na uchumi imara na WA one boxing ni kazi ya kuwapa utajiri sio sehemu ya kutafutia pesa ya kula
 
Kuna yule Ras alikamatwa kwenye wizi usiku akadundwa akafa.
Thomas Mashali, hakuwa Mwizi alikataa kulipa 3000 ya bodaboda akataka kutumia ubabe boda akaita mwiziii mwiziii raia kuja wakafikia mwilini mwa Thomas mpk wanakuja kugundua ni Mashali mtu kashachakaa
 
Back
Top Bottom