Kauli ya J. Kikwete unawafundisha wana CCM tuwe wakweli

Kauli ya J. Kikwete unawafundisha wana CCM tuwe wakweli

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Mhe. Rais Mstaafu J. Kikwete ameandika katika ukurusa wake wa Twitter maneno haya;

Ndoto ya wananchi nikuona vijana wanapata ajira na maslahi yanayoendana na Hali ya uchumi ya Sasa. Nikipata nafasi yakuzungumza na Rais sitasahau kumweleza haya.

Je, Mzee anawashwa Kama akina Hapi, Makonda na vijana wa CCM walivyotuaminisha miaka michache iliyopita? Au yupo sahihi kwamba maslahi na ajira nikipaumbele Cha vijana?
 
Kubana ajira ni moja ya mistake kubwa mno za jiwe , sjui hata wanaomsifu huwa wanamsifu Kwa lipi ? Bora Mungu alimpumzisha Kwa Amani mana alikuwa anakuja kuondoka Kwa riots na ingekuwa disaster Kwa nchi
 
Kikwete ni Kiongozi! Hivyo ana wajibu wa kumshauri kiana Mama Samia kufuata nyendo zake, badala ya kuangukia kwenye udikteta na utawala wa hovyo kama uliopita.
 
Samia ajitenge mbali sana na hawa wanafiki. Angekuwa na chembe ya ukweli angetujulisha wale waliosomba pesa ya escrow kwa magari ya Ikulu walikuwa kina nani.

Hata hivyo, nina hakika hiyo haitakuwa tweet ya Kikwete.
 
Kutotoa stahiki hata kwa wafanyakazi ( madaraja, increments, rikizo na madai mengine) kwa wakati ni jambo linalokwaza sana
Wafanyakazi walimwachia Mungu
Pale Mbeya Mei Mosi fulani hali ilikuwa mbaya watu wakasema basi tuendelee na kazi
Ila kiukweli iliboa
 
Mkuu mbona kwenye alaunti yake hakuna ujumbe kama huo
 
Samia ajitenge mbali sana na hawa wanafiki. Angekuwa na chembe ya ukweli angetujulisha wale waliosomba pesa ya escrow kwa magari ya Ikulu walikuwa kina nani.

Hata hivyo, nina hakika hiyo haitakuwa tweet ya Kikwete.
Utatengwa wewe kapuku,hoa wakubwa achana nao wanajuana wenyewe
 
Ni Haki yake kama mwananchi kuongea kama anaona jambo halipo sawa...

Ni Busara kama ana sikio la kiongozi kumshauri pale anapoweza...,

Ni kupotoka kama taifa kudhani kwamba maendeleo yataletwa na mtu mmoja..., bali inabidi tujenge system endelevu kwa kujumuisha wadau wote..., kazi za viongozi ziwe ni kuhakikisha mipango hio endelevu inaendelea sio kuja na mipango yao kutoka God Knows Where....
 
Huyo mzee akubali kuwa kashastaafu aache kuwashwawashwa kila zama na kitabu chake mbona mwinyi ni mkimya huyo.mzee mbona hatulii aisee !nikirejea hotuba yake chato akizikwa jpm inanipa hasira sana !we mzee ebu pumzika aliyepo.anawasaidizi.wake watamshauri nchi itaenda zama zako umeme kukatika twiga kubebwa bandari rafiki zako walijimilikisha escrow n.k mbona HUKUSHUGHULIKIA HAYO SAHV UNATAKA USHAURI LINI ANGALI KIPINDI CHAKO KILA SIKU UMEME KUKATIKA NA KUTANGAZIWA MAJI YAMEPUNGUA?*****?
 
Amsaidie kwenye tax base na collection kabla kuanza kuahidi ajira ....makusanyo sio stable akiongeza ajira na mishahara atapasuka mama wa watu aende taratibu
 
Allah ampe maishe marefu[emoji116]
IMG-20210403-WA0003.jpg
 
Back
Top Bottom