Kauli ya Joh Makini baada ya kuambiwa kapotezwa kimuziki

Kauli ya Joh Makini baada ya kuambiwa kapotezwa kimuziki

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,772
Reaction score
22,598
Bio Pofile 600x898 Joh Makini.png

MWANAMUZIKI ambaye hivi karibuni aliachia wimbo wake uitwao Mipaka, John Simon ‘Joh Makini,’ amefungukia kupotezwa kimuziki na baadhi ya wanamuziki wanaofanya vizuri kwamba si kweli, bali wanaosema hivyo hawafuatilia vizuri muziki wake.

Akichonga na Full Shangwe, Joh alisema kwamba kabla ya watu kuzungumzia juu ya kupoa kwake kimuziki, tofauti na kipindi cha nyuma inabidi waangalie kazi anazofanya na nini kilimfanya asikike sana kuliko wakati huu.

“Si kweli kwamba nimepoa kama ambavyo watu wanakuwa wanazungumza huko kwenye mitandao, mimi bado nipo vizuri na kazi zangu zinafanya poa, zaidi sitegemei kuchuja hata siku moja,” alisema Joh.

Muungwana
 
Watu wa Arusha wanadai Joh Makini ni mshamba
 
Nilishangaa ule wimbo ft Aka hakuwekea nguvu mara perfect combo chali akatoa wimbo ft Davido niliuckia mara moja tu.

Hawa wasanii wa hip hop wabongo wangekuwa serious wangekuwa ndo wanakimbiza game la hip hop Africa sijui wapoje maana ukickia hip hop ya Nigeria ni vichekesho tupo ukiilinganisha na ya Tz
 
John alikuwa anabebwa na beef kati yake na ngosha fid lakin toka fid amkatae jamaa kapotea kinoma

Alitoa ngoma na davido kama hakijatokea kitu (in edu boy voice)

London boy
Na Huo ndo Ukweli jamaa Kapotezwa mbaya na FID Q!
 
John alikuwa anabebwa na beef kati yake na ngosha fid lakin toka fid amkatae jamaa kapotea kinoma

Alitoa ngoma na davido kama hakijatokea kitu (in edu boy voice)

London boy
Wewe utakuwa ndo edu boy mwenyewe
 
Macho na midomo yake kama sio mzima huyu.. yaani ana swaga flani za mashaka mashaka sana
 
Wenyewe wakihojiwa wanasema eti "Wameswitch".., bila kutuambia kuwa " Wameswitch " On au Off!!!
 
John alikuwa anabebwa na beef kati yake na ngosha fid lakin toka fid amkatae jamaa kapotea kinoma

Alitoa ngoma na davido kama hakijatokea kitu (in edu boy voice)

London boy
wasukuma mchelewa kuja mjini ...ndo maana Tz nzima mnaonekana kama watu wa ajabu.
 
Wenyewe wakihojiwa wanasema eti "Wameswitch".., bila kutuambia kuwa " Wameswitch " On au Off!!!
Tatizo nyie mashabiki wa hip hope ngumu ...niwanafiki ...msanii akiimba ngumu amumsaport...akiimba nyepesi Akauza sana mnaanza kumponda...mjue mnzingua.
 
Tatizo nyie mashabiki wa hip hope ngumu ...niwanafiki ...msanii akiimba ngumu amumsaport...akiimba nyepesi Akauza sana mnaanza kumponda...mjue mnzingua.
Mkuu mbona unanilisha Maneno? Mimi sio Shabiki wa Hip hop ila ni Shabiki wa Mziki Mzuri, album nilizokuwa nanunua ni za Juma nature wa Ugali, Prof Jay na Jay Mo wa Mvua na Jua.., sio huyu Jay Mo wenu alieswitch!!!
 
Back
Top Bottom