Kauli ya Kinana inaonyesha CCM imechoka amani

Kauli ya Kinana inaonyesha CCM imechoka amani

Naona Wachangiaji wengi hapo juu kwenye thread hii mmekuwa ''victim'' wazuri mliolengwa na mtoa mada!!! nahisi mmezidiwa na ama UCCMQUINE au UCHADEMAQUINE... kwa jinsi nilivyomsikia Kinana hana tofauti na wanachadema, na makundi mengine ambayo yamechangia baada ya rasimu ya katiba kutoka. YAANI HAWAKUBALIANI NAYO KWA ASILIMIA 100!!! sasa tatizo liko wapi? au ndo hivyo tena mkuki kwa binadamu mchungu?....Tafakari kabla ya kuamua...
 
Kwanza Kinana ana sababu millioni za kusema hayo, chache ni hizi:-
1: Rasimu ya Katiba inatoa uhuru zaidi kwa wananchi kuchagua na kuchaguliwa katika ngazi mbalimbali kitu ambacho chama chake hakitaki. Inataka chama kiwachagulie wananchi kiongozi.

2: Viongozi waliomo CCM sasa wana weza kupinga maamuzi ya chama kama yanakwenda kinyume na matakwa ya wananchi bila kubanwa na viongozi wahafidhina ndani ya chama.

3: Kwa Tume Huru, CCM inaweza kushindwa na mirija yao ya kunyonya nchi ikakatwa. Ujangili na rushwa za mikataba ukadhibitiwa.

4. Siri nyingi za kunyonya Taifa zitajulikana na wananchi hawata taka kusikia kitu kinachoitwa CCm.

5. Huduma nyingi za seriklai zitakuwa bure kama madawa na elimu, kodi nyingi za kinyonyaji zitafutwa na wanachi watafurahia maisha kuliko ilivyo sasa.

6. Huduma nyingi kama upatikanaji wa viwanja, umeme na maji itakuwa rahisi na urasimu utatoweka, itawarahisishia maisha raia.

7. Wakimbizi walio iteka serikali hawata ruhusiwa kushika nyadhifa za uongozi serikalini kwa usalama wa Taifa.

8. ...
 
Kinana anaenjoy kung'oa meno ya tembo tu. sasa CCM inag'olewa meno bila ganzi na Katiba mpya, anahofu kuloose control ya kudhibiti wabunge wao na viongozi ambao wanaweka maslahi ya watanzania mbele.
 
ana sababu zake yeye na chama chake,naamini hiyo rasimu ingetoa mwanya mkubwa wa uwindaji wa tembo wala asingesema hayo......aende zake.

Na bado tunahitaji rasimu hiyo inolewe zaidi. Raisi asiteue viongozi wa mihimili mingine. Nafasi za uwaziri, makatibu wakuu, Mwanasheria mkuu, Mkuu wa Polisi (IGP), Mkaguzi Mkuu wa Serikali n.k. zitangazwe na wale wenye sifa waombe kiisha kufanyiwa interview. Raisi apelekewe majina matatu kwa nafasi iliyotangazwa na ateue miongoni mwa hao kiisha apeleke jina bungeni kwa kuidhinishwa. Huu ndio uteuzi shirikishi unaoashiria kuwepo utawala bora.
 
Kinana: Hatuungi rasimu ya katiba kwa 100%. Hii ni kauli ya Kinana kama ilivyoandikwa na magazeti mengi ikiwemo lile la Nipashe. In fact, ameitisha kikao cha CC kujadili rasimu hii na kutoa msimamo.

Kwa kauli kama hii, ina maana kuwa ama anakataa maoni ya wananchi kwa asilimia 100 ambao ndio waliyatoa na yakafanyiwa uchambuzi na kuwekwa kwenye summary ikatoka hii rasimu, au ana maana kuwa wajumbe wa kuandika rasimu hii walitoa yao moyoni wakaandika bila kufuata maoni ya wananchi. Mimi sidhani kuwa wajumbe wa katiba walitoa yao kichwani, hapana bali walifanya uchambuzi wa yale ambayo ni maoni ya wananchi. Hivyo, kauli ya Kinana kuwa kwa asilimia 100 % CCM inaipinga rasimu hii maana yake kubwa ni kuwa CCM haitaki maoni ya wananchi na hivyo inataka mambo yaendeshwe kama anavyojua yeye Kinana na sio maoni ya wananchi. Hii ni dharau kubwa na udikiteta wa hali ya juu.
CCM hasa Kinana anajua kuwa kwa rasimu hii, wananchi wanakuwa washirika wakubwa katika kujiamulia mambo yao ndio maana wana uwezo wa kumpumzisha mbunge ambaye hafanyi yale waliyomtuma bungeni. Hii inajuikana kabisa kuwa, wabunge wa CCM wengi kwa sababu mara nyingi bungeni wameonekana kuwa hawawakilishi wanachi bali wanawakilisha chama. Hii rasimu inaongeza uwajibikaji wa wabunge kwa sababu, mbunge anaweza akafukuzwa chama na akaendelea kuwa mbunge. Ina maana kuwa watu kama Filikunjombe hawataogopa tena kuikosoa serekali wakihofia kufukuzwa chama. Hivyo ni dhahiri kuwa kuna uwezekano mkubwa wa wabunge wa CCM wakawa mwiba kwa CCM yenyewe kwa manufaa ya wananchi.
Kauli ya Kinana inaonyesha dhahiri kuwa CCM inataka kuendeleza udikiteta na hivyo isipopingwa vikali, inaweza ikaleta machafuko nchini. Kumbuka, wajumbe pale ambao wanaegemea upande wa CCM ni kama 80 % ya wajumbe wote ikiwa ni pamoja na mwenyekiti, mwenyekiti msaidizi na katibu. Na bado ushaihidi uliotolewa na Tundu Lissu bungeni unaonyesha ukaribu wa tume kwa mwenyekiti wa CCM. Bado Kinana anasema haikubali kwa 100%.

Waacheni wananchi waamue! Tumechoka kuamuliwa na watu wachache

Alitaka iruhusu ujangili,ufisadi,matumizi mabaya ya madaraka n.k.
 
Watanzania tumejichelewesha wenyewe,CCM haiko tayari kuliendeleza taifa...hata hii katiba ni unafiki tupu,ccm haina dhamira ya dhati..

Nakuunga mkono, Ukichukua lenz ukajaribu kukuza kilichopo mbali utagundua hii rasimu ya katiba inaweza kuwa mbaya zaidi kuliko iliyopo.
Wananchi walipendekeza baadhi ya vitu na kweli ni vizuri, Lakini pia wajanja wanatumia mwanya huo kuhakikisha wanakuwa na mianya kadhaa ya kuwalinda na kuwatunzia mali ghafi zao. Angalia suala la Serikali 3, Unadhani mwananchi wa kawaida anajua nini maana ya serikali 3, Faida na hasara zake?. Hilo ni dili fulani tu na wala siwezi kuamini ni mawazo ya wananchi waliowengi.
Halafu kumbukeni kwa wale ambao wamewahi kuwa makatibu na waunganisha taarifa, unaweza ukaacha mawazo ya mengi na ukachukua wazo hata la mtu mmoja kwa interest fulani tu. Ndicho kinachotokea hapa.
Unadhani kwa nini Serikali haiko tayari kupitisha kura kwa wananchi juu ya muungano?. Kura nyingi aidha muungano uvunjike au iwe serikali moja.
Think beyond spoken and what you see.
 
Back
Top Bottom