Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA na mgombea nafasi ya Uenyekiti, TunduALissu akizungumza kupitia clubhouse usiku huu amesema, kauli ya Mhe. Ezekiel Wenje hazina ukweli wowote na kwamba hamdai hata shilingi moja na hajawahi kumkopesha.
"kama anasema alinikutanisaha na huyo Abdul basi yeye ni dalali, anasema tulikutana mwezi Oktoba sio kweli mimi nilirudi Tanzania mwezi Novemba hayo aliyozumza hayana ukweli wowote" amesema Lissu na kuongeza kuwa.
"Katika hili niseme wazi hapa, kama kweli nimewahi kuomba msamaha kwenye Kamati Kuu kuhusu suala hilo la Abdul kama Wenje alivyosikika akisema, niombe watoe hadharani ile video nzima iliyokuwa inarekodiwa kikaoni pasipo kuihariri jambo lolote kama watathubutu kufanya hivyo, kwa kuwa walirekodi ili itumike kama ushahidi wa kuondoa sintofahamu kwa umma, mimi napendekeza iwekwe hadharani ama hata sauti tu umma usikilize halafu umma wenyewe utasema umeelewa nini kuhusu chama chao kilipofika na kinapoelekea kama ni salama ama sio salama chini ya watu hao hao watakaosikia uchafu wao".