Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
"IGP Mstaafu, Omary Mahita kusema wanasiasa wanaingilia jeshi. Tumekuwa tukisema siku zote kwamba sasa hivi vyombo vyetu vya ulinzi na usalama, mwananchi wa kawaida hawezi kuchora mstari kusema hapa ni Chama Tawala na hapa ni Polisi na Idara ya usalama.
"Yeye anaona vyote sawa. Hiyo ni hatari kubwa sana. Ni lazima ufanye raia aone kwamba jeshi la Polisi litatenda haki bila kujali mwananchi amebeba kadi ya chama gani cha siasa.
"Lazima ujenge mazingira ambayo Idara ya usalama wa Taifa itapeleka taarifa dhidi ya mwananchi za ukweli bila kujali kadi ya chama ambacho mwananchi anacho. Kwa sasa sivyo! - Zitto Zuberi Kabwe, Kiongozi Mstaafu wa ACT WAZALENDO
Soma: IGP Mstaafu Mahita: Jeshi la Polisi la Sasa linaingiliwa na Wanasiasa