Kauli ya mbunge Sugu kwamba CCM inachukua watu "Wajinga wajinga" kutoka CHADEMA siyo ya kiungwana

Kauli ya mbunge Sugu kwamba CCM inachukua watu "Wajinga wajinga" kutoka CHADEMA siyo ya kiungwana

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Nimemsikia mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi aka Sugu kupitia ayo tv akidai alipigiwa simu na Katibu mkuu wa CCM Dr Bashiru Ally ili ajiunge nao lakini amemkatalia.

Sugu amedai kuwa sura yake siyo ya CCM na kwamba wanaohamia chama tawala ni wale Wajinga wajinga.

Hizi lugha za kihuni hazipaswi kutumiwa na wabunge wamwachie Hajji Manara.

Maendeleo hayana vyama!
 
Kama mazuzu. Mi sijawahi kuona waliohama wakiwa wachangamfu. Wanakuwa wamezubaazubaa kama wamekamatwa ugoni au kama Waethiopia waliokamatwa Morogoro. Ni kama wanatupiwa nguvu ya giza fulani. Bahati mbaya sina picha.
 
johnthebaptist, Mjinga ni yule anashawishi ujinga kufanyika, katika hili KK hakwepi sifa hii. Nenda Tanzania Visiwani nenda sehemu yoyote ile kwenye siasa makini za ushindani, huwezi kukuta ujinga kama huu wa kuwanunua wapinzani wako ili waunge juhudi.

Upuuzi huu umeandikwa kwa wino wa "kinyesi cha kitimoto" ambao watoto na wajukuu wao watakuja kuwadharau daima, upuuzi ambao waasisi wa taifa letu ijapokuwa walikuwa ndio waasisi wa CCM, lkn katu wasingelithubutu kuutenda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom