Kauli ya mbunge Sugu kwamba CCM inachukua watu "Wajinga wajinga" kutoka CHADEMA siyo ya kiungwana

Wana kuwa tayari washakatwa mikia ili waingie zizini
Kama mazuzu. Mi sijawahi kuona waliohama wakiwa wachangamfu. Wanakuwa wamezubaazubaa kama wamekamatwa ugoni au kama Waethiopia waliokamatwa Morogoro. Ni kama wanatupiwa nguvu ya giza fulani. Bahati mbaya sina picha.

In God we Trust
 
Na yule mkuu wa nchi wa zamani aliyewaita wateule wake wa ngazi ya juu kabisa kuwa ni malofa, wapumbavu, ulimwambia aachane na lugha za kihuni amuachie Manara?.
 
Katika hali ya kawaida, mtu mwenye akili, hata ile ya kawaida tu, huwezi kukubali kununuliwa kama gunia la maharage.

Kwangu walikuja kundi la viongozi wa CCM wilaya, wakasema kuwa nikikubali kuungana nao nitakuwa mgombea pekee kupitia CCM kwenye ubunge, niliwajibu kiungwana lakini kwa uthabiti. Hawakurudia tena. Wamebakia kuwasumbua ndugu zangu kuwa wanishawishi. Lakini nao majibu yao yamekuwa waxi - kwani ninyi huwa hammwoni anaporudi likizo?

Sioni ubaya kwa chama kushawishi, ndiyo siasa zenyewe. Ni vibaya pale ambapo mtu akikataa, anafanywa adui.
 
Alichosema Sugu, kama ni kweli wanatongozwa na wao kukubali, hao ni malaya wa kisiasa na wanachofanya ni tabia ya umalaya malaya alioizungumzia Baba wa Taifa.

Ila sio wote wanaohamia CCM wametongozwa,
Kuna makundi matatu ya wahamaji kutoka Chadema kwenda CCM.
1. Wanasiasa malaya malaya waliotongozwa wakatongozeka, hawa ni watu wa hovyo na hawana maana hata huko CCM, japo wamepokelewa lakini wanadharaulika.

2. Men of principles, hawa ni wanasiasa mature, wanaojua siasa ni nini, walijiunga Chadema kwa sababu ya principles fulani, walipobaini Chadema imeachana na hizo principles nao wakaiacha kundi hili lina kina Masha, Dr. Slaa, Professor Safari and the likes, kamwe hutawasikia wakiibeza Chadema.
3. Survivors, hawa ni wasaka fursa, wasaka tonge na gold diggers ambao wamajitambua kuwa jahazi la Chadema linayumba and soon litazama, hivyo Chadema hakuna fursa tena mambo yote sasa ni CCM, hivyo kuliko kusubiri wazame jumla, wameamua to jump ships kujiokoa, to survive, na kusaka fursa.

Nasisitiza wasibezwe.


P
 
Kama ninyi ni wajinga kubalini tu. Wala sio dhambi
 
Mkuu acha kufananisha kinyesi cha kitimoto na huo upuuzi wa CCM

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ana haki ya kikatiba ya kujieleza.

Neno ujinga ni sifa, si tusi.

Hata Nyerere alilitumia katika hotuba.

Sasa na Nyerere naye alikosa uungwana?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nimeirekodi hiyo. Siku akiunga mkono juhudi za Jiwe, tutamtumia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…