Mimi ni mwanachama wa chama cha Mapinduzi CCM kindakindaki lakini ninaamini katika demokrasia, uchaguzi huru na wa haki katika kuijenga nchi na umoja wa kitaifa. Nimesikitishwa na kauli ya Waziri Nape kuwa matokeo yana tegemea anayehesabu na kutangaza matokeo ya kupiga kura na uchaguzi na siyo sanduku la kura.
Kauli kama hii inapingana na falsafa ya CCM ya 4R inalenga kurejesha Umoja uliomomonyoka kipindi cha awamu ya 5, kipindi cha JPM ambapo hata yeye amesahau kuwa ni mhanga na aliathirika na utawala huo,alipaswa aongoze kutetea haki,demokrasia na utawala bora.
Matokeo ya Uchaguzi 2019/2020 yalikosa uthamani na maana kiasi ya kuwa na Bunge lenye Taswira ya chama kimoja na bado upinzani tumesaidia kuungozea nguvu nje ya Bunge hatukuweza kuuzika tujifunze, Kauli ya Nape kisiasa ina maanisha kuwa CCM haina uhalali wa kutawala, kisheria ilivunja katiba na haizingatii maadili ya uchaguzi.
Si kweli, kauli kama hizi ni za dharau na huchochea machafuko. Nape amezoea kuropoka asome mazingira ya kisiasa kwa sasa. Akiwa kama kijana mwanasiasa anayetarajiwa kwa baadaye ajifunze kuzungumza kwa busara na hekima bila kukichafua chama. Makamu Mwenyekiti wa CCM ametumia muda mwingi sana kuwasihi vyama vya upinzani na wananchi kuwa safari hii hayatatokea madhaifu kama ya 2019/2020. Na kuwataka warudishe imani kwa chama cha CCM.
Pia Rais akaja na 4R ambazo alizitetea mbele ya mabarozi nchi za nje kuwahakikishia wawakilishi hao kuwa uchaguzi utakuwa wa huru na haki. Tusikubali ccm kuingia kwenye mtego huo. Tumesikia akina Msigwa nao wakilalamikia michezo michafu upande wa pili. Sisi ni chama kiongozi tuongoze kwa mifano bora. kujenga imani ya wananchi ni kazi kubwa kuliko kuibomoa. Kwa sasa wananchi wengi wanaweza kuacha kujiandikisha wakiamini matokeo ya uchaguzi tayari yameishapangwa kama yale ya 2020.
Dr Kitima alisema tutasambaratisha nchi kwa hali hii. Tusimkwaze mama yetu ambaye amejidhihiri ni mcha Mungu wa kweli na mwana demokrasia wa kweli duniani.
Pia soma==>> Kuelekea 2025 - Nape Nnauye: Kauli ya "Matokeo ya kura inategemea nani anahesabu na nani anatangaza" ilikuwa ni ya utani