Kauli ya Nape imenisononesha hata kama ni utani

Tatizo la watz hawapendi kuambiwa ukweli,Nape ameongea kinachofanyika miaka yote
 
Ufisadi kwa serikali ya ccm hautaisha hadi wauze kila kitu.

Kwani wana nyenzo muhimu za kuwabakisha madarakani na hata waboronge vipi hamna cha kuwafanya.
 
Pole Pole alishasema "Uchaguzi ukiwa Huru na Haki basi CCM wajiandae kupisha Ikulu" ni Hamphrey Pole Pole sio MIMI sio Nape Nnauye narudia "Uchaguzi ukiwa Huru na Haki basi CCM wajiandae kupisha Ikulu" alisema Pole Pole enzi hizo kwa hio Nape Nnauye alichofanya ni kuteleza ulimi Ila amesema ukweli kwamba bila kuchezesha matokeo na kumlipa refarii (Msimamizi wa Matokeo) CCM haiingii Ikulu

Sijui unamuelewa Nape Nnauye ? Yaan alimaanisha bila kuchezesha matokeo kwenye 1 weka 10 kwenye 10 weka 100 na kuja na matokea ya mfukoni CCM Ikulu itaisikia kwenye bomba
 
Haya maneno ya NAPE yapigwe screenshot au yawe copied yatunzwe, ya Kikwete akiwaonya ccm kwenye mkutano mkuu kutotegemea polisi, maneno ya Magufuli kuwa nikuteue mimi, nyumba nikupe na gari halafu umtangaze mpinzani, ya Samiah kuwa hata msipoipigia ccm itaunda serikali na ya Mkapa kwenye kitabu chake kuhusu wizi kwenye chaguzi,maneno ya Bashiru kubaki madarakani kwa kutegemea vyombo vya dola,na Mwenezi Polepole,Abdulhaman akikiri uchaguzi kuharibiwa 2019/2020 nk halafu yatunzwe ikibidi kitungwe kitabu kitachoelezea hali ya chaguzi zetu TZ na kunukuu yote hayo itakuwa ni ushahidi na vielelezo tosha kwa baadaye. Aidha,kama ni kweli kuna wizi kwenye chaguzi,Je hali hii mpaka lini? kwa muskabali wa nchi yetu.
 
Baadae ipi Mzee kwa hiki kizazi au kizazi kijacho?
 
Hakuna cha 4R hapo! Hiyo haiwezi kuifanya CCM isiibe kura.
 
Kosa la Nape ni kusema ukweli tu
 
Nani kasema ukweli kati ya Makalla na Nape
 
Daah sas yanini kwenda kupiga kuraa lnachosa... Sema hii nchi ngumu maana naona kama upinzani wako kimya na ndo mda wa kuchukua point
 

Nape kasema ukweli, hakuna mcha Mungu mwizi wa kura. Kama angekuwa mcha Mungu kweli angeruhusu tume huru ya uchaguzi. Unasema kutakuwa na uchaguzi wa haki, ila tume ya uchaguzi inabaki vile vile?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…