Kauli ya Rais ambayo ni sheria ni ipi?

Kauli ya Rais ambayo ni sheria ni ipi?

Kama Allen Kilewella weka ndani[emoji51]
Achapwe viboko hadharani na akitoka achapwe viboko 12 akumuonyeshe mkew
Kama…… mikutano ya siasa, kwa sasa isubiri mpaka wakati wa uchaguzi ujao! IKAWA HIVYO!
...Kila M'bunge na Diwani, ni marufuku kufanya mkutano nje ya eneo lake! IKAWA HIVYO!
.. ..Kama mtu anashambulia askari wenzie walioko FRONTI, basi huyo anajua kitakachompata! JAMAA AKALA SHABA MCHANA KWEUPEEEE!
 
Niliwahi sikia siku moja yule Mwandishi wa habari wa wizara ya afya akisema "kauli ya rais ni sheria" nilipo fuatilia taaluma yake ni mwanasheria nikasema ama kweli Bongo land tusha vuka viwango vya ujinga Sasa Ni upumbavu
 
Kweli viongozi wa kitaifa wanapaswa kudhibiti kauli zao. Nyingine zinatumika vibaya na nyingine zinaleta mgongano.

Mfano kauli ya hayati JPM ya walioshi kama malaika wataishi kama mashetani na kinyume chake, imekuwa mwiba kwa zama za leo.

Maana kwa sasa walioishi kama mashetani enzi zake, wamekuja na nguvu zote ili kurejesha walichopoteza. Na wale wengine kwa sasa kila kukicha afadhali ya jana!
 
Niliwahi sikia siku moja yule Mwandishi wa habari wa wizara ya afya akisema "kauli ya rais ni sheria" nilipo fuatilia taaluma yake ni mwanasheria nikasema ama kweli Bongo land tusha vuka viwango vya ujinga Sasa Ni upumbavu
Taahira huyo! Yalijipendekeza kwa jiwe Sana!
 
Kila siku huwa tunaambiwa na wapenda mamlaka ya Rais kwamba "Kauli ya Rais ni Sheria".. Hivi kauli ya Rais ili iwe sheria inatakiwa iwe na vigezo vipi ama kila akisemacho Rais ni sheria!!??
Mkuu Allen Kilewella, umeuliza a very valid question, na hili ndilo lile swali nililo liulizaga mahali, kuna baadhi ya kauli za viongozi zinatolewa kwa mamlaka gani na kwa sheria gani?.

Jambo hili niliwahi kuliendeshea darasa humu AG, Mshauri Mh.Rais Atoe Maagizo kwa Presidential Decrees Kuyapa Nguvu ya Kisheria

Ili kauli ya rais kuwa sheria, kauli hiyo baada ya kutolewa kwa mdomo, hufuatiwa na maandishi, kisha inaandikiwa a presidential decree na kutangazwa kwenye gazeti la seikali ndipo inakuwa sheria!.

P.
 
Kama…… mikutano ya siasa, kwa sasa isubiri mpaka wakati wa uchaguzi ujao! IKAWA HIVYO!
...Kila M'bunge na Diwani, ni marufuku kufanya mkutano nje ya eneo lake! IKAWA HIVYO!
.. ..Kama mtu anashambulia askari wenzie walioko FRONTI, basi huyo anajua kitakachompata! JAMAA AKALA SHABA MCHANA KWEUPEEEE!
Na kesho Rais Samia akitoa kauli kwamba mikutano ya kisiasa sasa ruhsa, hutakiona chombo chochote cha dola, hasa polisi, kikizuia tena hiyo mikutano.

Kauli ya Rais wa Tanzania ni sheria kwani ukiihoji, chochote kile kinaweza kukutokea kama ilivyotokea kwa Watanzania waliothubutu kuhoji kauli hizo.

Kauli ya Rais wa Tanzania haizingatii Katiba aliyoapa kuiheshimu, kuilinda na kuitetea inasemaje. Hivyo kauli ya Rais Samia iko juu ya Katiba ya nchi.

Na kibaya zaidi kauli ya Rais hivi sana imeshuka ngazi hadi kwa wateule wake. Mradi wewe ni kiongozi wa serikali ama chama, kauli yako itatafsiriwa hivyo.

Kwa Tanzania chochote kile kinaweza kufanyika na wananchi wakakaa kimya kwa woga kama wa kondoo mbele ya fisi. Na huo ndio ukweli mchungu.
 
Niliwahi sikia siku moja yule Mwandishi wa habari wa wizara ya afya akisema "kauli ya rais ni sheria" nilipo fuatilia taaluma yake ni mwanasheria nikasema ama kweli Bongo land tusha vuka viwango vya ujinga Sasa Ni upumbavu
Tumeshavuka viwango vya ujinga!!??
 
Ili kauli ya rais kuwa sheria, kauli hiyo baada ya kutolewa kwa mdomo, hufuatiwa na maandishi, kisha inaandikiwa a presidential decree na kutangazwa kwenye gazeti la seikali ndipo inakuwa sheria!.

P.
Asante sana Pasco.

Haya maelezo yako na bandiko lako ni kitu cha muhimu sana. Nani anafuatisha!!??
 
Back
Top Bottom