"Tulipoingia madarakani mwaka 2005 tulifanya mambo mawili muhimu kuhusu mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu. Kwanza uamuzi kwamba, mikopo itolewe kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya umma na vile visivyokuwa vya serikali. Kabla ya hapo ilihusu vyuo vya umma pekee. Pili kwamba, kila mwaka tuongeze fedha zinazotengwa kwa ajili ya Mfuko huo ili idadi ya wanafunzi wanaonufaika iongezeke. Tulikuta Mfuko ukiwa na shillingi billioni 56.1 unanufaisha wanafunzi 16,345 mwaka 2005. Tukaongeza kila mwaka na katika mwaka huu wa fedha (2012/13) tumetenga shillingi bilioni 345 zinazowanufaisha wanafunzi 98,772."
Badala ya kukata aya moja ingependeza zaidi kama ungeweka hotuba nzima hapa ili yote ichambuliwe. Otherwise, ngoja na mie nikate aya yangu. lol.
Rais anasema kuwa "Tanzania ni kubwa kuliko Kenya na Uganda kwa eneo na idadi ya watu lakini ndiyo tuliokuwa na idadi ndogo ya wanafunzi kwa ngazi zote hizo. Kwa mfano, mwaka 2005 idadi ya wanafunzi waliokuwa Chuo Kikuu nchini Kenya ilikuwa 108,407, Uganda 88,360 na kwa baadhi ya nchi za SADC kama vile Afrika Kusini idadi hiyo ilikuwa 717,973.
Wakati wenzetu wakiwa na idadi hiyo, sisi tulikuwa na wanafunzi 40,719 tu katika vyuo vikuu nchini. Hali ilikuwa hivyo pia kwa elimu ya sekondari. Kenya ilikuwa na wanafunzi 925,341, Uganda 619,519 na Afrika Kusini 4,186,882 wakati Tanzania ilikuwa na wanafunzi 524,325 tu waliokuwa katika shule za sekondari."
Rais anaendelea kusema kuwa:
"Tuliona hali hii haikubaliki hivyo tukaamua hatuwezi kuiacha iendelee. Tukaamua kudhibiti. Tukachukua hatua tulizochukua za kupanua elimu katika ngazi zote… "
"Kufuatia juhudi hizo, idadi ya wanafunzi waliopo kwenye vyuo vikuu nchini imeongezeka sana, kutoka wanafunzi 40,719 mwaka 2005 hadi wanafunzi 166,484 mwaka 2012. Kwa upande wa sekondari mwaka 2011 tulikuwa na wanafunzi milioni 1.79 na wenzetu wa Kenya walikuwa na wanafunzi milioni 1.77. Haya ni mafanikio makubwa."
Kwanza, ukiangalia Rais ameanza huko nyuma kwa kufanya analysis nzuri huku akilinganisha na nchi nyingine. Lakini aliposema kuwa idadi ya wanafunzi waliopo kwenye vyuo vikuu nchini imeongezeka sana, hakufanya tena analysis kwa kulinganisha na nchi alizozitaja mwanzoni.
Swali langu ni vipi huko Kenya, Uganda na Afrika Kusini namba imebakia ile ile ya mwaka 2005 au nako kumekuwa na idadi kubwa ya wanafunzi? Kama nako kumeongezeka, kweli tunaweza kujivunia kuwa tumefanikiwa? Kenya na Uganda pamoja na kuwa wachache si bado watakuwa wametupiga bao tuu?
Pili Rais anazungumzia zaidi quantity bila kughusia kabisa quality ya elimu, which is the very concern ya matokeo ya form 4 yaliyopita.
Tatu hizo bilioni 345 ni kwa ajili ya wanafunzi 98,772 kati wanafunzi 166,484.
Speech ya Rais ilikuwa na gaps ambazo zinaleta maswali zaidi ya majibu.