Kauli ya Rais Kikwete...

Hiyo ni changamoto, lazima itafutiwe ufumbuzi.

Vilevile tukumbuke kuwa wanaojiunga chuo kikuu sio watu fresh from form six peke yao.

Mkuu, mature entry ni wachache sana kwa sasa, unless wafanye kampeni ya kuhamasisha watu wakasome first degree kwasababu kuna mabilioni ya mkopo na watoe full mkopo. Still kwa msururu wa vyuo, ni wazi as from 2015 kutakuwa na changamoto nyingi na hasa vyuo binafsi vinavyotegemea vicent vya tuition fee kujiendesha.

Kuna sababu za msingi kuoanisha mipango inayofanywa kwenye sector ya elimu. Mambo yasifanywe kwa matamko ya kisiasa na ahadi za mabwana wkubwa wa world bank na IMF.

Kwamfano, sio lazima kufanya enrollment kubwa sana kutoka primary kwenda secondary ili tu kuonyesha umefikia MDG. Matokeo yake ndo haya, unapeleka takataka secondary ambako hata mwalimu hayupo.
 
Hiyo ni changamoto, lazima itafutiwe ufumbuzi.

Vilevile tukumbuke kuwa wanaojiunga chuo kikuu sio watu fresh from form six peke yao.
Hao wa 'mature age entry" au "in-service" una takwimu ni asilimia ngapi ya wadahiliwa wote?
 

Badala ya kukata aya moja ingependeza zaidi kama ungeweka hotuba nzima hapa ili yote ichambuliwe. Otherwise, ngoja na mie nikate aya yangu. lol.

Rais anasema kuwa "Tanzania ni kubwa kuliko Kenya na Uganda kwa eneo na idadi ya watu lakini ndiyo tuliokuwa na idadi ndogo ya wanafunzi kwa ngazi zote hizo. Kwa mfano, mwaka 2005 idadi ya wanafunzi waliokuwa Chuo Kikuu nchini Kenya ilikuwa 108,407, Uganda 88,360 na kwa baadhi ya nchi za SADC kama vile Afrika Kusini idadi hiyo ilikuwa 717,973.

Wakati wenzetu wakiwa na idadi hiyo, sisi tulikuwa na wanafunzi 40,719 tu katika vyuo vikuu nchini. Hali ilikuwa hivyo pia kwa elimu ya sekondari. Kenya ilikuwa na wanafunzi 925,341, Uganda 619,519 na Afrika Kusini 4,186,882 wakati Tanzania ilikuwa na wanafunzi 524,325 tu waliokuwa katika shule za sekondari."

Rais anaendelea kusema kuwa:

"Tuliona hali hii haikubaliki hivyo tukaamua hatuwezi kuiacha iendelee. Tukaamua kudhibiti. Tukachukua hatua tulizochukua za kupanua elimu katika ngazi zote… "

"Kufuatia juhudi hizo, idadi ya wanafunzi waliopo kwenye vyuo vikuu nchini imeongezeka sana, kutoka wanafunzi 40,719 mwaka 2005 hadi wanafunzi 166,484 mwaka 2012. Kwa upande wa sekondari mwaka 2011 tulikuwa na wanafunzi milioni 1.79 na wenzetu wa Kenya walikuwa na wanafunzi milioni 1.77. Haya ni mafanikio makubwa."

Kwanza, ukiangalia Rais ameanza huko nyuma kwa kufanya analysis nzuri huku akilinganisha na nchi nyingine. Lakini aliposema kuwa idadi ya wanafunzi waliopo kwenye vyuo vikuu nchini imeongezeka sana, hakufanya tena analysis kwa kulinganisha na nchi alizozitaja mwanzoni.

Swali langu ni vipi huko Kenya, Uganda na Afrika Kusini namba imebakia ile ile ya mwaka 2005 au nako kumekuwa na idadi kubwa ya wanafunzi? Kama nako kumeongezeka, kweli tunaweza kujivunia kuwa tumefanikiwa? Kenya na Uganda pamoja na kuwa wachache si bado watakuwa wametupiga bao tuu?

Pili Rais anazungumzia zaidi quantity bila kughusia kabisa quality ya elimu, which is the very concern ya matokeo ya form 4 yaliyopita.

Tatu hizo bilioni 345 ni kwa ajili ya wanafunzi 98,772 kati wanafunzi 166,484.

Speech ya Rais ilikuwa na gaps ambazo zinaleta maswali zaidi ya majibu.
 

Nadhani changamoto nyingine inayotukabili ni gap kubwa kati ya maamuzi ya kitaalam na ya kisiasa. Tunahitaji wataalam wetu wafanye tafiti na kuziandika ili watunga sera na wananchi waweze kuzisoma. Hiyo itawezesha kuzalisha sera ambazo ziko supported by research. Sasa hivi tunatumia sana tafiti zilizofanyika nchi nyingine ambazo mazingira yake sio lazima yawe yanashabiiana na Tanzania.

Bila vyuo vikuu na wasomi kushiriki bega kwa bega jitihada zinazofanyika hazitazaa matunda kwa wingi tunaotarajia.
 
Ni kweli mkuu,

Hata hivyo ili tufanikiwe ni LAZIMA wataalam na utaalam uheshimiwe na wataalam watambue wajibu wao kwenye ujenzi wa taifa. Tulipo sasa kila lawama anatupiwa mwanasiasa as if nchi haina mtaalam hata mmoja.

Tatizo wataalam wetu wameachwa pembeni kabisa ndio maana hata wasomi wanaingia kwenye siasa. Tumejijengea utamaduni mbaya sana - wa ku-import solutions hata kwa mambo yaliyowazi. Kila kitu ni consultant au mwekezaji. Tunakuwa kama hatujiamini.

Lakini utashangaa ukiende nchi jirani, mfano Rwanda, utakuta mambo mengi wametoa hapa Tanzania. Hata wataalam wao wengi wamesoma hapa. Sasa sisi kwa nini hatutumii utalaam wetu!?
 

Mkuu,

Ni kweli nimechukua kipande cha hotuba. Hapa JF ukiwawekea watu maandishi marefu hawasomi. Ndio maana nimechagua sehemu moja ndogo ya hotuba.

Asante kwa kuileta hotuba ya Rais kwa urefu wake.

Ni bayana kuwa Rais anapotoa hutuba huwa na mambo mengi sana ya kuongea na wananchi wake. Lakini hotuba ndefu mno pia hufanya wasikilizaji wakose somo lililokusudiwa kwa muda uliopangwa. Hotuba ya Rais haiwezi kusema yote.
Gap inayobaki ni ya wachambuzi.

Nilitegemea wasomi wetu na waandishi wa uchambuzi wafanye analysis ya hotuba ya Rais na kuweka data za jinsi namba hizo zilivyobadilika Kenya na Uganda. Hiki ndicho tunachokikosa hivi sasa, pundits...
 
Ni kweli mkuu,

Hata hivyo ili tufanikiwe ni LAZIMA wataalam na utaalam uheshimiwe na wataalam watambue wajibu wao kwenye ujenzi wa taifa. Tulipo sasa kila lawama anatupiwa mwanasiasa as if nchi haina mtaalam hata mmoja.

Tatizo siyo kuwa lawana wanatupiwa wanasiasa bali wanasiasa wanadhani wanaweza kutatua kila tatizo hata yale ya kitaalamu.

Wataalamu wapo wengi tuu na wangependa watu wanufaike na utaalamu wao lakini sidhani kama wanapewa hiyo nafasi.

To make the matter even worse, wataalamu nao wameamua kuwa wanasiasa.

Hapa sina maana ya wataalamu wa propaganda za siasa wanaojaribu kuuaminisha umma.
 

Tatizo la wasomi wetu ni kwamba hawafanyi kitu kama hawalipwi posho. Hata ukitaka kumfundisha mtu ujuzi mpya, atakuuliza posho ya semina sh. ngapi. Wenzetu Ulaya wanalipia kuweza kuhudhuria semina za kujifunza mambo mapya, sisitunalipwa ili tujifunze. Aliyeleta tabia hii kairoga vibaya sana nchi yetu!!!

Kungekuwa na wasomi wanajitoa kufanya jambo fulani na jamii inawafahamu, basi hata siku kukiwa na fungu rasmi la shughuli hiyo inakuwa rahisi kuwaconsult. Sasa msomi kajifungia ofisini mpaka siku akisikia kuna fungu ndio anasema hiyo kazi anaiweza, at the same time anakuja mgeni ambaye anakuonyesha kazi alizozifanya na matokeo yake. In the end unakuta consultant wa nje anapewa kazi. Wasomi wetu wajifunze kujitoa ili kazi zao zionekane na wapewe kazi zaidi.
 

Really? I thought tunaongelea mambo ya msingi yasiyotakasiasa za maji taka hapa kwenye hii thread.

1) muswada wa maji dar ulitupwa na nani?na ulitupwa kwasababu maji yanatoka kwa wingi dar au?

2) muswada wa mitaalaulitupwa na mitaala ikaletwa baada y sikukadhaa na bado ikaundiwa tumekuichunguza.....hayo sio mambo ya maendeleo?

3) uzuiaji wa mianya ya wizi wa fedha za umma waziwazi au kwa kificho including kuchukua hatua za kisheria kwa wezi. Hii si maendeleo?au ni mdundiko?

4) discussions around health system in this country - focusing on quality and not quantinty of health facilities. Lakini kiongozi wako haelewi, anaona kujenga zahanati kila kijiji ndo maendeleo, wakati leohii kuna health centre wala sio dispensary, ina watumishi watatu na mmoja ni clinician na wengine ni atendants?

5) pikipikiambulance.....nenda kwenye health facilities za mikoa ya Kigoma, Mara, manyara.....kaangalie uone jinsi hizo pikipikizilivyokuwa mapambo tangu zipelemwe huko. Hii ni mipango janjajanja, ya hovyo kabisa. Mipango inayopangwa na washikaji wakati wanakunywa gin and tonic na wanapeana deal. Tulisema huu ni mradi wa kipuuzi, tujipange tuanze kunuua ambulance kidogo kidogo. Nyie mkatuona machizi.

Sasa hapo nani anaongelea maendeleo na nani anaongelea Mduara na Segere?


Wewe unaongea mambo gani? Au unaona kwavile tunaamua kupuuzia posts zenu zisizo na mashiko, basi mnaona mnaweza kubwabwabaja tu mnavyotaka?

Chukua na hii ukamwambie kiongozi wako kwamba wakina mama wa Kishapu wana enjoy maji safi na salama.

 

Kuna "hang-over" ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010. Hii hang-over imekuwa protracted mpaka sasa. Kwa sasa ni too late kuiondoa, inabidi tuishi nayo mpaka 2015.

Uchaguzi umeisha tangu 2010 lakini watu bado wanaendelea na kampeni. Lakini as we will be approaching 2015 ni wajibu wetu kukumbushana kuwa uchaguzi ukiisha tuendelee kujenga nchi.

Ile tabia ya kwamba mwisho wa uchaguzi mmoja ni mwanzo wa uchaguzi mwingine itaua taifa.

We can not afford to live in campaign atmosphere for 5 more years..
 

Umeona kama huyu.

Hawa ndio mfano wa watu ambao bado wako kwenye kampeni tangu mwaka 2010. Wataendelea hivi mpaka mwaka 2015 na tusiposimama kidete kuwakumbusha wataendelea tena mpaka 2020. Kamwe hatutakuwa na muda wa kufikiri kama taifa nini tunafanya, nini tufanye, nini tusifanye.

Kwasasa watu wa namna hii inabidi tuwavumilie tu, ila baada ya 2015 kama taifa ni lazima focus iwe kwenye kujenga nchi tu.
 

Waandishi wenyewe si unawajua?

Hata hivyo, Rais akitoa speech ambayo ina gaps ina maana anampa the President in waiting nafasi ya kumnil down.

Fortunately kwake, hutunaga a president in waiting na sijawahi kusikia the leader of the opposition akirespond speech ya Rais hasa zile za kila mwezi.

Nonetheless, a presidential speech should be good and sold.

Of course there are many things to deal with, but ni better speech iwe short as a mini skirt lakini i-cover the essential parts.

To be fair kwa Rais, inabidi kuwe na improvement kwenye speech zake. Kwa mfano, anapodai kuwa kwa upande wa sekondari mwaka 2011 tulikuwa na wanafunzi milioni 1.79 wakati waliofanya mitihani wa kidato cha nne mwaka uliofuatia asilimia zaidi asilimia 60 (should I say zaidi ya asilimia 90?) wamefeli makes one wonders.
 

Hakuna smart opposition or to be more precise serious opposition.

Kipindi hiki ambacho form four wameeli kwa kiasi kikubwa ilikuwa ni mda muafaka kwa opposition kuuza sera zake za elimu (kama wanazo sera bora). Huu ungekuwa wakati wa kuzaungumzia blueprints za opposition education policy. Lakini unapoona solution inayotolewa na opposition ni kuwaambia wanafunzi waandamane ni LAZIMA ujiulize, are these guys serious about their readiness to govern? what practical solutions do they offer?
 

Usilie, ani unataka kutafuta sympathy kutoka kwake?

Sasa hivi fucus ipo wapi?
Serikali haina focus, hata pale inapokumbushwa kwama angalieni mmeweka mpango wa miaka mitano lakini kuna important lines haziawa costed kwenye budget haishtuki, inaleta kejeli za siasa na kupiga makofi.

Then unasema tuache mpaka 2015 ndo tuseme basi.
 

Nchi haiwezi kuwa kwenye focus kama kampeni zinaendelezwa non stop. Hakuna sheria inayokataza kufanya kampeni non stop lakini tunajichelewesha wenyewe kuendelea kwa kudwell kwenye bickerings...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…