Kauli ya Rais ni Sheria! Hii kauli ilitokea wapi?

... duh; kwamba Rais ni nusu Bunge; na ile nusu nyingine inakamilishwa na Spika na wabunge. Kwamba, ile nusu ya Spika na wenzie inatunga sheria na nusu ya pili ya Rais nayo inatunga sheria kwa matamko! Hatari sana.
 
Basi kama ni hivyo, kauli za rais ziwe ni pendekezo la marekebisho ya sheria, zipelekwe bungeni zikapitishwe kwa kufuta sheria na kanuni ya kudai malimbikizo ya kodi. Mtu akifanikiwa kutokulipa kodi katika muda uliotakiwa basi iwe imetoka hiyo tugange kodi zijazo, halafu tusikilizie utamu wake!!!
 

Yes ndio maana mabadiliko yoyote ya sheria lazima yapate kibali cha Rais na muswada uundwe na wataalam wa wizara husika then waziri anapeleka bungeni, na ukipitishwa unarudi tena kwa Rais kusainiwa ili iwe sheria sasa! Bila Rais kuruhusu hamna muswada unaenda bungeni, tofauti kabisa na nchi zingine ambapo mbunge au kikundi cha wabunge kinaweza kuandika muswada na kuupeleka bungeni, ukipata kibali cha spika unasomwa, na unaweza kuwa sheria. Haya yaliasisiwa na awamu ya kwanza lakini bado yana mashiko kidogo kwa kutazama quality ya wabunge wenyewe.

Hivi nani kati ya wabunge wa magu anaweza kutengeneza muswada wa sheria? hata kama wangekua na uwezo huo, hawa macomedian kweli wanaweza kitu? Wanachuma tu na kuwekeza binafsi muda wao uishe wajaribu tena!
 
Ipo kwenye biblia!
Inasema,'neno la mfalme ni sheria' .....
Ukisoma habari za Daniel utanikuta hii,kitabu Cha Daniel!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…