ubongokid
JF-Expert Member
- Apr 30, 2017
- 2,154
- 4,184
Kwanza niseme wazi kabisa kwamba Naelewa na kuamini kwamba kauli ya Mheshimiwa RAIS iliakisi kile ambacho yeye kama Samia Suluhu Hassan anakiamini na anakifahamu ila hakikuakisi kile ambacho RAIS anafahamu. Sisemi hivi kwa lengo la kumtetea bali nataka tu niaze mjadala huu katika namna ambayo ataakisi kile ambacho ninataka kusema.
Napenda sote tufahamu kwamba kuna Samia Suluhu as a person na Kuna Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. URAIS ama RAIS ni taasisi ambayo msimamizi wake Mkuu ni Mtu ambaye anaitwa Samia Suluhu Hassan.
Mtu huyu anao wajibu wa kikatiba na kimaadili wa kusimamia Taasisi ya URAIS na taasisi zote ambazo zinawajibika chini ya mamlaka ya URAIS. Hivyo basi anapotia Kauli yake kama Samia Suluhu Hassan anatakiwa atambue kwamba UHURU huo hana. Yeye kama RAIS kauli yake inawakilisha taasisi ya URAIS na bila kujali mtazamo wake ni lazima kauli yake ipimwe kwa mizania ya URAIS.
Swali la kujiuliza JE, SAMIA SULUHU HASSAN anawafahamu ambao wanafanya matukio haya ya utekaji na uuaji wa watu? Jibu rahisi la swali hili ni kwamba yeye kama Samia Suluhu hawafamu Ila yeye kama Taasisi ya URAIS huenda anawafahamu na Kama Taasisi ya Urais haiwafahamu wanaofanya matendo haya basi Taaisi bado inao uwezo wa kuwafahamu watu bila shida wala shaka yoyte ile.
Jambo lingine ambalo nataka sasa nileweke sawa ni kuhus athari za kauli ya Samia kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama. Katika Tasnia ya Serikali, uongozi na uwajibikaji kuna kitu kinaitwa IMPUNITY-Ile hali ya mtu kutokuwajibishwa anapofanya makosa.
Kauil ya Mheshimiwa Dr. Samia ama kwa kukusudia au kutokusudia imeweka mazingira ya Vyombo vya ulinzi na Usalama kuwa na impunity. Madhara yake tumeanza kuyaina ikiwamo ni wananchi kukosa imani na vyombo vya ulinzi na usalama.
Madhara yake yatachukua muda sana kubadilika. Kwani sasa hivi vyombo vya Ulinzi na Usalama vinatazmwa kama Genge la Wahalifu. Jambo hili ni baya sana hasa tunapoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu maana kuna uwezekano mkubwa sana Vyombo vya Ulinzi na Usalama vikawa Targeted kwa sababu tu ya wananchi kukosa imani nao pamoja na serikali wanayoiwakilisha.
Nina mambo mengi sana ambayo ninaweza kumshauri Mheshimiwa RAIS kama Taasisi ili ayafanye mapema ili kutuliza hali ya mambo. Ila kwa sasa Ushauri wangu ni rahisi tu. Clean The House.
Soma Pia: Rais Samia: Mauaji ya Kibao hayakubaliki. Uchunguzi umeanzishwa