Kauli ya Serikali kuhusu Uwanja wa Mkapa kwa mechi ya fainali ya Simba Vs Berkane

Kauli ya Serikali kuhusu Uwanja wa Mkapa kwa mechi ya fainali ya Simba Vs Berkane

Nilishangaa jinsi adhabu ya Simba ya kucheza mechi mbili bila mashabiki ilivyobadilisha ndani ya muda mfupi sana na kuwa adhabu ya mechi moja.

Naamini pamoja na uzembe wa hali ya juu uliofanyika, uamuzi wa CAF utabadilishwa na mechi itarudi kwa Mkapa.

Kuna namna ambavyo Simba inajua kuongea kikubwa ikasikilizwa.
 
Huyo jamaa anajua CAF ni Watanzania kwamba anaweza kuwapiga kamba tu?
 
Kama wanazipenda sana hizi timu wangehakikisha huu uwanja unakuwa vizuri muda wote,

Ni zaidi ya kununua magoli na kutoa ndege!
 
Msigwa bora akae Kimya maana issue ya Uwanja wa Amani ishakuwa official,CAF wenyewe jana wametangaza kila timu imepewa barua. Maana kama anawaongeza watu hasira.
Mkuu wana maudhi sana hawa viumbe
 
Halafu unashajaa jitu limo humu, lishabiki la Simba au Yanga, halafu linashabikia CCM. Mamaaaee!! Mchawi wa hii nchi ni hilo chama chakavu.
 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa ametembelea na kukagua maendeleo ya ukarabati wa Uwanja wa Benjamin Mkapa na kuridhishwa na hatua ya marekebisho na ukarabati wa miundombinu, ufungwaji wa viti vipya, uboreshaji wa vyumba vya wachezaji, uboreshaji wa vyumba vya waamuzi na uboreshaji wa eneo la kuchezea (Pitch) na mpaka sasa ukarabati umefikia asilimia 85 na ubora wa uondoaji maji ndani ya uwanja umeongezeka mara kumi zaidi ya kabla.

View attachment 3334873
Aidha pia serikali kutoa Zaidi ya billion 650 kwa ujuenzi wa viwanja vipya viwili ikiwemo kiwanja cha Dodoma na Arusha na hatua ya ujenzi wa uwanja wa Arusha umefikia asilimia 43 na pia uwanja wa Uhuru utaboreshwa kufikia kiwango Cha Kimataifa.
View attachment 3334837

VIDEO: ITV Tanzania
Aache sound za ajabu. Yeye ana utaalamu gani wa kukagua uwanja?!
 
Tunashukuru mkandarasi kuchelewesha marekebisho hawa wapakwa mafuta wangeutia gundu na mbuzi zao 😃😃😃😂😂... Mechi n Aman stadium hutaki nenda Bodi ya ligi
1747328447070.jpg
 
Msigwa anajitekenya mwenyewe kisha anacheka

Kilichobaki hizo pesa walizopiga kwa kisingizio cha kukarabati uwanja warudishe na hizo nafasi zao wajiuzulu mara moja
 
Nilishangaa jinsi adhabu ya Simba ya kucheza mechi mbili bila mashabiki ilivyobadilisha ndani ya muda mfupi sana na kuwa adhabu ya mechi moja.

Naamini pamoja na uzembe wa hali ya juu uliofanyika, uamuzi wa CAF utabadilishwa na mechi itarudi kwa Mkapa.

Kuna namna ambavyo Simba inajua kuongea kikubwa ikasikilizwa.
CAF sio TFF
CAF sio bodi ya ligi

Hii mechi haitorudi kwa Mkapa labda wanaocheza nao wasiwe Barkane
 
Back
Top Bottom