Abdul Nondo
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 520
- 2,930
Kutoka kauli ya vijana mjiajiri hadi kauli ya vijana kuwa wezi na kutokuwa waaminifu.
Kwa ujumla wake hakuna mtu aliyefurahishwa na kauli zako Mh.Ndugai dhidi ya vijana ukiwashambulia Bungeni kwamba hawaaminiki,wana kiwango kidogo cha uwaminifu ukifafanua kwamba wakipewa mradi wasimamie wanaiba na kufilisi.
Shutuma ulizotoa dhidi ya vijana kutokuwa na uwaminifu ni maoni yako na hayana uhalisi wowote sababu hakuna utafiti wowote uliofanywa kuthibitisha kwamba vijana ndio kundi au rika lisilo na uwaminifu kama usemavyo wewe.Bila kujali ni vijana katika kundi gani uliokuwa unawazungumzia ,tunaamini shambulio kwa kundi moja la vijana ni shambulio kwa vijana wote nchini (An attack to a single group of youth,it is an attack to all youth countrywide).
Ni aibu kubwa kuona Spika wa Bunge , kiongozi wa muhimili mkubwa wa Bunge , kusimama na kushambulia vijana kwamba ni wezi na hawana uaminifu.
Kama spika wa Bunge ambaye ni kiongozi wa muhimili mkubwa nchini ulipaswa kufahamu kwamba vijana ndio kundi kubwa ambalo halithaminiwa na serikali na hata bunge lililo chini yako limeshindwa kuisimamia serikali kikamilifu ili changamoto wanazopitia vijana zipatiwe ufumbuzi.
Vijana unaowashambulia ndio ambao wanahitimu kila mwaka kuishia mtaani na wengine bila kuajiriwa au kujiajiri.Wewe na Bunge lako mmeshindwa kuisimamia serikali kikamilifu kuweka mazingira wezeshi kwa sekta binafsi kuajiri vijana,kujiajiri au serikali kuajiri.
Vijana unaowashambulia ndio ambao kila kuchwa Bunge lako limekuwa likitumika kupitisha sheria kandamizi zinazoumiza vijana na kuhatarisha maslahi ya vijana.
sheria ya Bodi ya mikopo (Makato).
sheria ya makosa ya mitandao.
kanuni ya maudhui mtandaoni.
sheria ya huduma za habari.
sheria na kanuni ya fao la kujitoa(withdrawal benefits), leo hii kijana akifukuzwa ajira /kazi hawezi kupata mafao yake yote isipokuwa 33.3% ya mshahara wake tuu.
Hujawahi kupinga sheria hizi kama Spika, leo unawaita wezi wasio na uwaminifu.
Vijana unaowashambulia ndio ambao wamekuwa watiifu na wanyenyekevu katika makambi mbalimbali ya JKT wakizalisha ,wakiongeza nguvu kazi katika ujenzi wengine wanajenga Ikulu Dodoma ,kulima , wakifunzwa ukakamavu na kufundishwa kushika silaha ila hatimaye wengi wao makundi na makundi wamekuwa wakirudishwa nyumbani, na kwa ujuzi wao wa kushika silaha ila bado nchi ipo salama.Hujawahi kuwatetea kama Spika leo unawaita wezi wasio na uwaminifu.
Vijana unaowashambulia leo ndio ambao mara zote mmekuwa mkiwatumia na kuwarubuni kwenye kampeni zenu za kusaka ubunge wakiamini mtakuwa watetezi wao Bungeni kumbe ndio mnawageuka na kuwashambulia kwamba ni wezi na hawana uwaminifu.
Vijana unaowashambulia leo ndio ambao wanakumbana na mateso na manyanyaso viwandani wakitafuta riziki , wanakumbana na changamoto nyingi chini ya mkandarasi YAPI katika mradi wa SGR ila hawachoki ,wanafanya kazi bila mikataba katika daladala na mabasi ya mikoani ila hawachoki kutafuta riziki, Bodaboda wakikumbana na uonezi na faini za trafiki.Hujawahi kuwatetea kama Spika leo unawaita wezi wasio na uwaminifu.
Vijana unaowashambulia ndio ambao wamejazwa magerezani kama mahabusu kesi zao zisizo na dhamana haziishi upelelezi ,miaka na miaka wakiwa ndani kwa kesi za kumbambikiwa , hujawahi kuwatetea kama Spika wa bunge,ila leo unawaita wezi na wasio waaminifu.
Vijana unaowashambulia ndio ambao waliwekeza fedha zao katika korosho hatimaye serikali ikazikwapua zote ila kama spika ulikaa kimya ,ndio ambao wanalima na kuzalisha bila upatikanaji wa masoko ya uhakika ya mazao yao,mfano huko mkoa wa Songwe,wilaya ya Songwe mmewakataza vijana kuuza ufuta wao nje ya wilaya yao ,mnawalazimisha mfumo wa stakabadhi ghalani kupitia minada, hujawahi watetea ila leo unawaita wezi na wasiowaaminifu.
CAG ametoa ripoti ya ubadhilifu na wizi katika Wizara,Halmashauri na sekta mbalimbali za serikali . Spika Ndugai athibitishe wizi huu na ubadhilifu umefanywa na vijana ili kuhalalisha shutuma zake dhidi ya vijana kwamba ni wezi na hawana uwaminifu.
Nadhani kama nchi kuanzia bunge na serikali mnajukumu la kutatua changamoto za vijana kuliko kuwatupia shutma za wiza na kutokuwa waaminifu.
Abdul Nondo.
17.Aprili.2021