Kauli ya Tulia juu ya Mamlaka aliyonayo Rais wa nchi haikuja kwa bahati mbaya, ni fadhila baada ya kuhakikishiwa

kasenene

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2008
Posts
1,632
Reaction score
2,413
Kwa jinsi alivyozungumza Tulia (NS) jana wakati wa kuapishwa viongozi/Mawaziri wapya ni dhahiri shahiri kuwa aliandaliwa makusudi kuongea vile baada ya kuhakikishiwa nafasi ya "Mzee wa nina file milembe mimi"'.

Ili halina shaka kabisa na ni wazi, ndio maana badala ya Tulia kuzungumzia yanayohusiana na tukio la jana yeye alijikita zaidi katika kuupotosha uma juu ya mamlaka aliyonayo Rais unapolinganisha na ile mihimili mingine miwili yaani Bunge na Mahakama....akubumshwe tu kuwa kuna msemo walinena Wahenga kuwa ukiona mwenzako ananyolewa basi na wewe tia maji.

Asipopewa uspika Tulia naacha kuandika Jamii kuanzia leo.
 
Haya bana wenye nchi wanatuendesha wanavyotaka, lakini?
 
Submission to Executive speech!👇😁😁😁
Mambo ya aibu yanatokea katika nchi yangu Tanzania👆😑😑😑
 
Kwa hali ya kawaida tu kwa miaka kadhaa kiti kimekuwa kikiachwa kwa naibu. Labda lolote linaweza kutokea kwenye siasa
 
Tumeshachoka na drama..ingekuwa kaseti tunge fast foward mpaka 2025
 
Sio suala la kuhakikishiwa tu, pengine ni kujipigia mstari.!
 
Huu ndio ukweli ambao hata Dr John Magufuli aliuweka hadharani.

Rais sio tu Head of Executive, pia ni head of State haiwezekan Dunia Nzima Rais akawa sawa na Spika na Jaji Mkuu kimadaraka.
 
Bunge na Rais wote Wana NGUVU sawa. Rais anaweza KULIVUNJA Bunge na Bunge linaweza KUMUONDOA Rais MADARAKANI.

Kwenye hii video hapa chini Tulia anajaribu kuwapotosha Watanzania kuwa mhimili wa urais ni mkubwa kuliko mihimili mingine kitu ambacho siyo sahihi.

Tulia anajua ukweli ila anachojaribu kufanya ni "kumhonga" Rais kwa kumuonyesha kuwa atajisalimisha kwake(Submission) ili achaguliwe kuwa Speaker wa Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwani anajua kuwa hapa Tanzania Rais ana influence kubwa katika uchaguzi wa Speaker wa Bunge.

Unaweza kujionea mwenyewe jinsi tulivyo na katiba mbovu.Imagine anaechagua Speaker wa Bunge ni Rais na wala siyo Bunge na ndiyo maana Tulia ameanza kujipendekeza kwa Rais mapema ili apate nafasi hiyo.

Taifa haliwezi kuendelea kwa mihimili ya nchi kumwabudu na kumtumikia Rais.Tunahitaji katiba ambayo itaipa mihimili separation of power.
View attachment 2077923
Anachojaribu kufanya Tulia ni kuuza mhimili wa Bunge ili tu asikose tonge na ndiyo maana hata alichukua form za kugombea usipika bila ya kujiuzulu kwanza unaibu speaker kitu ambacho ni kinyume na katiba yetu.Alifanya hivyo ili akikosa usipika basi aendelee kuwa naibu speaker.Ni mambo ya kupigania tonge.

Watu wa namna hii ambao wanatanguliza maslahi yao binafsi mbele badala ya kutanguliza maslahi ya Taifa mbele ni hatari sana kwa Taifa letu na ndiyo wamefanya nchi hii isiweze kufanya lolote la maana ndani ya miaka 60 ya uhuru.
View attachment 2077956
Wabunge CHAGUENI mtu ANAYEJUA MAMLAKA ya BUNGE.
 
Dunia nzima ndo hali ilivyo tofauti itakuja tu kama spika na Rais watatoka vyama tofauti.
 
Mkuu, Tulia ni mwanasheria nadhani.
 
Back
Top Bottom