Bunge na Rais wote Wana NGUVU sawa. Rais anaweza KULIVUNJA Bunge na Bunge linaweza KUMUONDOA Rais MADARAKANI.
Kwenye hii video hapa chini Tulia anajaribu kuwapotosha Watanzania kuwa mhimili wa urais ni mkubwa kuliko mihimili mingine kitu ambacho siyo sahihi.
Tulia anajua ukweli ila anachojaribu kufanya ni "kumhonga" Rais kwa kumuonyesha kuwa atajisalimisha kwake(Submission) ili achaguliwe kuwa Speaker wa Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwani anajua kuwa hapa Tanzania Rais ana influence kubwa katika uchaguzi wa Speaker wa Bunge.
Unaweza kujionea mwenyewe jinsi tulivyo na katiba mbovu.Imagine anaechagua Speaker wa Bunge ni Rais na wala siyo Bunge na ndiyo maana Tulia ameanza kujipendekeza kwa Rais mapema ili apate nafasi hiyo.
Taifa haliwezi kuendelea kwa mihimili ya nchi kumwabudu na kumtumikia Rais.Tunahitaji katiba ambayo itaipa mihimili separation of power.
View attachment 2077923
Anachojaribu kufanya Tulia ni kuuza mhimili wa Bunge ili tu asikose tonge na ndiyo maana hata alichukua form za kugombea usipika bila ya kujiuzulu kwanza unaibu speaker kitu ambacho ni kinyume na katiba yetu.Alifanya hivyo ili akikosa usipika basi aendelee kuwa naibu speaker.Ni mambo ya kupigania tonge.
Watu wa namna hii ambao wanatanguliza maslahi yao binafsi mbele badala ya kutanguliza maslahi ya Taifa mbele ni hatari sana kwa Taifa letu na ndiyo wamefanya nchi hii isiweze kufanya lolote la maana ndani ya miaka 60 ya uhuru.
View attachment 2077956
Wabunge CHAGUENI mtu ANAYEJUA MAMLAKA ya BUNGE.