Kauli ya vitu kupanda bei kisa vita ya Ukraine inapindishwa na walioielewa wanafunga mikanda kimyakimya

Kwa nini serikali haijatoa stimulus package kama mataifa mengine wanavyofanya, mishahara kwa wafanyakazi imeendelea kuwa kiduchu miaka nenda rudi huku hali ya maisha ikiendelea kupaa kwa kasi......wanachoweza kufanya ni kukamua tozo kutoka kwa wanyonge.
 
mafuta ya kula ya alizeti inayolimwa hapo Singidae yamepanda kutoka sh. 5000/6000kwa lita hadi sh. 9500kwa lita ndani ya wiki 2.

Utaambiwa Kisa vita ya Ukraine. Tena anayekwambia Ni Rais wa nchi. Tz shamba la bibi limerudi kwa kasi sana.
 
Hali ni mbaya sana, bidhaa zinzidi kupanda bei, gharama za usafiishaji bidhaa kuleta nchini pia zinazidi kupanda, ila kipato hakipandi kabisa.
 
Wakati yeye ndio anazidi kuhamasisha vitu vizidi kupanda bei. Anawakumbusha wafanya biashara wafanye hivyo.
 
Forest of words desert of points,mbolea imepanda kabla ata mawazo ya rusia na ukraine kutabiri kuwa watapigana yani kiufupi mbolea ilipanda siku magufuli wanamzika chato ,week moja baada ya mazishi ya jpm ngano tulinunua 1300 ikapanda mpaka 2000 pkg.
 
Wajinga wengi walizoea serikali laghai na ya kuongea uongo kama ya Magufuli.
We ndo mjinga number moja unayekaa kwa shemeji yako hujui ata bei mahitaji ta hapo nyumbani ya kila siku ni yalikuwa ni shilingi ngapi na leo shilingi ngapi.huo uongo wa magufuli unauonea wapi wakati ni maisha tunayoyaishi.!?
 
Maneno marefuuuu kama mnazi! Tunachotaka ni kwamba SSH ana mpango katika kutoa nafuu kwa wananchi kama vile kuweka subsidies kwa bidhaa muhimu kama mafuta - kama alivyofanya Kagame kwa wananchi wake?
Badala yake kaongeza tozo ya mafuta.
Kifupi mpango huo haupo, hata yeye amesema kupanda kwa bei serikali haihusiki na inabidi tuzoee tu. Mwenzake wa Zanzibar amepiga biti vitu visipande bei lakini huyu ye kavibariki vipande .

Hayati Mwenda alikua na u- Adolf Hitler lakini kuna vitu kweli asingeruhusu. Fikiria kua serikali ili subsidy gharama za kufunga umeme huyu Bibi kaja kaondoa hio subsidy. Sooner or later tutakuja kuambiwa kua hata Elimu bure haiwezekani tulipie tu.
 
Wakati yeye ndio anazidi kuhamasisha vitu vizidi kupanda bei. Anawakumbusha wafanya biashara wafanye hivyo.
Hapa sijamuelewa kabisa, hakutakiwa kusema hivi hadharani. Ni anahamasisha upandaji wa bei. Siku ile amezungumzia tu Tanesco kufunga umeme kwa TZS 27,000/= siku hiyo hiyo bei ikapanda. Mama haoni athari ya matamshi yake.
 
Maneno marefuuuu kama mnazi! Tunachotaka ni kwamba SSH ana mpango katika kutoa nafuu kwa wananchi kama vile kuweka subsidies kwa bidhaa muhimu kama mafuta - kama alivyofanya Kagame kwa wananchi wake?
Badala yake kaongeza tozo ya mafuta.
Vita ya Ukraine haiwahusu Zanzibar?
 
Vita ni kisingizio tu. Bali tumekwapua misaada na tozo kila kona kugharamia safari zisizo na umuhimu kwa Taifa. Hadi wauza mchaichai wamepandisha bei vita imehusikaje hapo
 
Hapa sijamuelewa kabisa, hakutakiwa kusema hivi hadharani. Ni anahamasisha upandaji wa bei. Siku ile amezungumzia tu Tanesco kufunga umeme kwa TZS 27,000/= siku hiyo hiyo bei ikapanda. Mama haoni athari ya matamshi yake.

Hafai ata kua kiongozi wa shule
 

Acha Kuwa kama mbuni mnyama. Embu niwekee statistics /takwimu za uagizaji wa bidhaa za Tanzania kutoka Russia na Ukraine.

Hakuna msiba usiokuwa na waliaji, sasa corona imekwisha kusingiziwa now ni Ukraine na Urussi na hata vita ikiisha itatengenezwa na sababu zingine
 
Bado nakazia, niliyemtaja kwenye mada hii kipindi hicho leo kaanza kazi ya kupotosha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…